Alibaba

samedi 4 mai 2013

Amwambia ingia Islam, nae kwa nini? kiyama chenu kimefika, chetu bado





AAWW, WAHESHIMIWA WASOMI WA FORUM abuchief.blogspot.com ajabu ya wanadam wa jana na leo kufanana, japo tunatofautiana kwa sayansi na elimu ya teknolojia ya hali ya juu, lakini ujinga wa asili bado unamtawala ila alierehemewa.
Mtiikisiko uliowakumba watu wengi duniani na waendelea kutokana na uongo wa uvumi wa kiyama na mwisho wa dunia, ulitushangaza sana. Sikitiko, baadhi ya waislam wamepatikana kaumini. Hii ni moja ya dalili za mwisho wa dunia.Je, hauoni? hausikii? haufikiri?.
Tumekumbwa na anasa za ulimwengu kwa kuzinunua au kuzitengeza.
Mfano: Internet imajaa wema mwingi vile vile uovu, wema ni elimu zenye manufaa, na uovu huo, ni kuendekeza filamu za makafiri hasa propaganda za KANISA kutoka Tanzania, Naijeria hadi Côte d'Ivoire, kwa ajili ya kuridhisha nafsi zenye kuamrisha maovu, au marafiki wabaya.
Vijana wetu wanaharibika au kuharibiwa akili na viwili wili vyao kwa kuuza na kuvuta unga, bangi, pombe musics n.k.
Mauti yanatushindikiza popote tuendapo , kitanzi kiko tayari shingoni, malaika mtoa roho yuko tayari, dalili kubwa za kiyama zatusogelea kwa kasi, moto wa jahannam unahamu ya kuwachoma waabuduo tamaa zao za mali za haramu na michezo mingine. Ibada hazitimizwi vema, jicho la ALLAAH limesahaulika. Nini kimebaki? kifo cha ghafla, kilio na kujuta bila faida.

Shituka.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire