Alibaba

samedi 3 décembre 2022

Brazil vs Cameroun Qatar 2022

.... Cameroon 🇨🇲 imekuwa timu ya kwanza kutoka Africa kuifunga Brazil kwenye tournament kubwa 🔥

Full 🕡 Cameroon 🇨🇲 1 - 0 🇧🇷 Brazil
90' + 2 🕡 Vicent Aboubakar ⚽
90' + 3 🕡 Vicent Aboubakar red card ♦️


😆 Aboubakar alipofunga goli akajisahau kama tayari ana kadi ya njano, akavua jezi, mwamuzi akampa kadi ya pili ya njano, akala umeme ♦️... Kisha  Mwamuzi na Aboubakar wakapeana mikono 🤝  Fair play  ♥️



⭕ Vicent Aboubakar ndiye mchezaji pekee mpaka sasa aliyeifunga Brazil kwenye michuano hii ya World cup 2022 🔥


⭕ Katika hatua ya makundi kwenye world cup 2022 🇶🇦 hakuna timu iliyoshinda mechi zote tatu. Hakuna timu yenye points (9) ! 😮

⭕ Aboubakar amekuwa mchezaji wa pili kufunga goli na kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo mmoja wa kombe la Dunia tangu 2006 alipofanya hivyo Zinedine Zidane.

Timu zilizofuzu kutoka mabara tofauti.

08 - Europe
02 - South America
02 - Africa
02 - Asia
01 - North America
01 - Australia
00 - Antarctica

NB : Mabara yote (6) ambayo wanaishi binadamu yameingiza timu kwenye 16 bora World cup 2022 Qatar 🇶🇦 🙌

dimanche 27 novembre 2022

Ray c atupia neno kuhusu Wema sepetu

Msanii wa kike wa muda mrefu katika muziki wa Bongo Flava, Rehema Chalamila maarufu Ray C ameweka neno lake baada ya Wema Sepetu kuposti Video ikimuonyesha akilia.
"Natamani siku uamue utoke hiyo nchi usafiri nchi ya mbaaaaaali japo kwa muda tu...ukutane na watu tofauti kabisa na uliowazoea, upate marafiki wapya watakaompenda wema kama binadamu siyo wema kama star, sababu wewe una roho nzuri sana na unajua kuishi na watu, unastahili kuwa na watu wenye upendo wa dhati kwako pia, you deserve it ma.❤love you always" ameandika Ray C.

RUSSIE: LÉNORME BAGARRE GÉNÉRALE ENTRE LE ZÉNITH ET LE SPARTAK MOSCOU, AVEC 16 CARTONS DONT 6 ROUGES

Le match de Coupe de Russie entre le Zénith Saint-Pétersbourg et le Spartak Moscou a basculé ce dimanche dans le chaos, avec une énorme bagarre générale en toute fin de rencontre. Malcom et Quincy Promes ont notamment été impliqués.
Un monde parallèle. Alors que la planète foot a les yeux rivés sur le Qatar, la Russie, mise au ban de toutes les compétitions internationales en raison de la guerre en Ukraine, vit elle au rythme de ses chocs domestiques, qui se poursuivent dans un certain anonymat. Ce dimanche, en même temps que le Maroc signait une énorme performance contre la Belgique à Doha, le Zénith Saint-Pétersbourg et le Spartak Moscou s'affrontaient ainsi devant plus de 50.000 spectateurs en Coupe de Russie. Un match qui a donné lieu à une "remarquable" bagarre générale.

En toute fin de partie, alors que le tableau des scores affichait 0-0, la rencontre - déjà tendue si l'on en croit les 10 cartons jaunes distribués - a soudainement basculé dans le chaos. Tandis que l'arbitre tentait (physiquement) de mettre fin à une altercation entre le Néerlandais Quincy Promes (Spartak) et le Colombien Wilmar Barrios (Zénith), des premiers coups de pied et de poing ont été échangés entre le Brésilien Rodrigao (Zénith) et le Jamaïcain Shamar Nicholson (Spartak). Avant que tout le monde ou presque ne s'y mette.
Pendant plusieurs dizaines de secondes, les joueurs des deux équipes et les membres des staffs ont réglé leurs comptes avec une violence rare dans le football professionnel. Il a fallu un long moment pour que le calme revienne, et que l'arbitre sanctionne ensuite cet instant de folie, en dégainant pas moins... de six cartons rouges: trois pour Wilmar Barrios, Malcom (l'ancien Bordelais) et Rodrigao côté Zénith, et trois pour Aleksandr Selikhov, Shamar Nicholson et Aleksandr Sobolev côté Spartak. Un Sobolev qui n'a pas volé son expulsion, compte tenu du nombre de coups qu'il a distribués 

full video link





Voici 7 parties s-nsibles de la femme que vous pouvez toucher pour la mettre dans l'ambiance.



1. Passez avec attention et délicatesse vos main dans ces cheveux. Passez doucement vos mains dans les cheveux de votre femme, tout en lui parlant tendrement avec un petit sourire au lèvre et vous verrez la suite elle va certainement apprécié. 2. Touché délicatement son bassin Le bassin est très proche du lieu que vous connaissez , c'est donc généralement un excellent moyen pour la stimuler. 3. La cuisse (côté intérieur) C'est aussi très spécial car il est proche du panda . Enchantez doucement ici et elle vous aidera à aller plus loin. 4. Massage réchauffant les pieds Cela permettra d'accomplir trois choses pour votre jeune femme: Premièrement, elle se sentira plus détendue et heureuse. Deuxièmement, elle sera vraiment gâtée et gâtée, et troisièmement, elle entrera dans l'état d'esprit de la chose. 5. Placez vos doigts sur l'arrière de vos genoux. 6. Avec tendresse glisser vos main derrière le dos Je dirai ou devrais dire que cela suscitera en elle des sentiments fous. Elle n'aura pas l'occasion de résister au déluge et à la paix que sa apporte. 7. Les S--.e.ins ( Vous savez de quoi je parle)

Là pas besoin de trop parler avec des touches tendre vous verrez vous même l'effet.

mercredi 23 novembre 2022

Timu za Taifa za England na Wales zimetangaza kuwa manahodha wao hawatovaa vitambaa vilivyoandikwa "OneLove"

Timu za Taifa za England na Wales zimetangaza kuwa manahodha wao hawatovaa vitambaa vilivyoandikwa "One Love" baada ya kupewa taarifa kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kupewa kadi ya njano mara tu watakapo ingia uwanjani.

Taarifa ya pamoja kutoka kwa Mashirikisho ya soka ya England 🇬🇧 , Wales ,Belgium 🇧🇪 ,Denmark 🇩🇰 ,Germany 🇩🇪 , Netherlands 🇳🇱 na Suisse 🇨🇭 imesema kuwa.. 






"FIFA imeweka wazi kabisa kuwa itatuwekea vikwazo vya kimichezo ikiwa manahodha wetu watavaa vitambaa hivyo uwanjani"

"Sisi kama Mashirikisho, hatuwezi kuacha wachezaji wetu wawekewe vikwazo,hivyo tumewaarifu Manahodha wasifanye hivyo katika mechi yoyote ya Kombe la Dunia"


"Tumechanganyikiwa na uamuzi huu wa FIFA ambao haujawahi kutokea, tuliwaandikia barua mwezi Septemba kuomba ruhusa ya kuvaa vitambaa hivi lakini hatukujibiwa."


dimanche 20 novembre 2022

Vivutio vikubwa Qatar kwa sasa ni Stadium 974

Moja kati ya vivutio vikubwa nchini Qatar ni uwanja wa 974 utakaotumiwa katika michezo ya Fainali za Kombe la Dunia 2022.


Upekee wa uwanja huo pamoja na mambo mengine ni kwamba baada ya Fainali za Kombe la Dunia 2022 utabomolewa na vifaa vyake kutolewa msaada kwa nchi zinazoendelea.


Uwanja huo umepewa jina la 974 kwa maana mbili kwanza ndio code ya kimataifa ya simu ya Qatar  pili umejengwa kwa idadi ya makontena 974 upo Doha Qatar na unachukua mashabiki 40,000, uwanja huu hauna AC kama vilivyo viwanja vingine.


Qatar world cup 2022



samedi 19 novembre 2022

Messi na Ronaldo kwenye picha ya pamoja

Watu wengi walihisi hii ni picha ya kutengenezwa sio uhalisia lakini sio kweli, hii ni picha ambayo imepigwa ikiwaonyesha wachezaji wakubwa kuwahi kutokea duniani Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakicheza mchezo wa ludo


Louis Vuitton LV ni kampuni ya kutangaza bidhaa za thamani kubwa sana ambayo imekuwa ikiwatumia mastaa mbalimbali kutangaza bidhaa zao.

Kupitia kurasa zao Messi na Ronaldo wote wamepost picha hii na kuandika caption moja wote.

La Victoria está en la Mente. Una larga tradición artesanal construyendo baúles fotografiada por @annieleibovitz para @louisvuitton.

Victory is a State of Mind. A long tradition of crafting trunks photographed by @annieleibovitz for @louisvuitton.

dimanche 13 novembre 2022

Kombe la Duniya 2022 : Nguruwe Marufuku

Wenyeji wa kombe la FIFA la Dunia mwaka huu nchi ya Qatar imeendelea na msimamo wake wa kukata kuingizwa bidhaa kama sex toys, matumizi ya pombe isipokuwa kwa mpangilio maalum.


Qatar pia wamezuia nyama ya nguruwe na endapo utabeba vyote vitabaki uwanja wa ndege na kwenye vizuizi na havitorudishwa kwa muhusika.

Licha ya kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja, pia wamezuia watu ambao sio wanandoa kufanya mapenzi na endapo utabainika utakumbana na kifungo cha miaka saba jela.

mwalim by Nuuru Salaam ( the light of Peace)

Raisi kwenda kuona World Cup

Rais wa Liberia George Weah amelifahamisha baraza la seneti kuwa anapanga kukaa siku tisa nchini Qatar kutazama mechi za kombe la dunia .

Bw Weah - mwanasoka wa zamani - aliondoka nchini wiki iliyopita kwa ziara kadhaa za kigeni, lakini sio mipango yake yote imefichuliwa.


Mwanawe Timothy, ambaye ni Mmarekani, atakuwa katika kikosi cha Marekani katika mashindano ya Kombe la Dunia, yatakayong'oa nanga tarehe 20 Novemba.

George Weah alichezea timu kubwa za Ulaya, zikiwemo AC Milan na Chelsea.


Rais huyo mwenye umri wa miaka 56 alibadili kazi na kuchaguliwa kuwa rais wa Liberia mwaka wa 2017.

Habari za mipango ya safari ya nje ya rais zimewakasirisha raia wengi wa Liberia, wengine wametumia vipindi vya kupiga simu kwenye redio na kwenye mitandao ya kijamii kumkosoa.


Wanasema itakuwa ni kutotilia maanani hali ya wananchi kwa rais kwenda Qatar wakati ambapo watu wengi walikuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la chakula, pamoja na kutokuwa na uhakika kuhusu mwenendo wa sensa ya watu iliyocheleweshwa sana, ambayo Bw Weah aliiahirisha hivi majuzi kwa mara ya sita.

Wafanyakazi wa Bw Weah - ambao hawajajibu maswali kuhusu gharama ya safari hiyo - wamejibu wakosoaji wake, wakisema ziara za nje za rais "zitazaa faida kubwa" kwa nchi.

lundi 7 novembre 2022

Refa katowa kadi nyekundu 10

Refarii kutoka Nchini Argentina ameweka rekodi ya aina yake baada ya kutoa kadi nyekundu 10 katika mchezo mmoja.


Refarii Facundo Tello ameingia kwenye vichwa vya vyombo vya habari Duniani baada ya kutoa kadi nyekundu kumi (10) katika dakika za mwisho wa mchezo wa kombe la Ligi Nchini Argentina 🇦🇷. Aidha, mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya (1-1) hadi dakika ya tisini (90) kisha kuongezwa dakika 30 ambapo Refarii Tello alitoa kadi hizo nyekundu kutokana na matukio yaliyotokea Uwanjani hapo baina ya klabu ya Boca Juniors ambao walipoteza mchezo huo dhidi ya Racing (1-2).

Refarii huyo ni miongoni mwa Waamuzi watakaochezesha kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Qatar na tayari ameshatoa kadi za njano 612 pamoja na nyekundu 45 huku akiwa amechezesha michezo 118 katika maisha yake ya Urefa.

mardi 1 novembre 2022

Davido afisha mtoto wake

Mtoto wa mwanamuziki Davido Adeleke na mpenzi wake Chioma Rowland, Ifeanyi Adeleke (3) amefariki dunia baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea ‘Swimming Pool’ nyumbani kwao.


Vyombo mbalimbali vya habari nchini Nigeria vinaripoti kuwa mtoto huyo alifariki jana Jumatatu Oktoba 31, 2022.


Taarifa zinasema Ifeanyi alizama kwenye maji kwa muda mrefu kabla ya wazazi wake hawajagundua kutoweka kwa mtoto wao na baadaye walikuta akielea kwenye maji.

Davido anakuwa msanii wapili nchini humo kumpoteza mtoto kwa kuzama kwenye maji, kwani mwaka 2018 moto wa msanii D’Banj naye alipoteza maisha katika tukio kama hilo.

jeudi 20 octobre 2022

Aonesha uchi wake ili kuziwiya Free kick

Beki wa Klabu ya Independiente Santa Fe ya nchini Colombia, Geisson Perea amewaacha mashabiki kwenye mshangao mkubwa baada ya kufanya kitendo kisicho cha kawaida katika mchezo wao dhidi ya Jaguares de Cordoba wikiend ya Oktoba 17, 2022.


Geisson Perea akiwa sehemu ya ukuta wa mabeki kuzuia mpira wa adhabu (free-kick) uliyokuwa sehemu ya hatari zaidi karibu na lango la goli lao, aliamua kutoa nje sehemu zake za siri ili kumchanganya mpigaji wa mpira bila mwamuzi kuona tukio hilo lililonaswa na kamera za uwanjani.


Kitendo hiko kimetafsiriwa kama njia ya kumchanganya mpigaji wa mpira huo uliyokuwa umetengwa na mwamuzi kuelekea katika milingoti mitatu ya timu yake.

Kupitia Win Sports TV, Geisson Perea amesema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuiweka sawa bukta yake na sio kujiweka hadharani kwa ulimwengu. Hakufahamu pia kuwa kamera zilikuwa zikimmulika yeye.

Kwa mujibu wa Dailymail mashabiki wametaka mchezaji huyo apatiwe adhabu kali kutokana na kitendo hicho ambacho ndani ya uwanja hakupatiwa kutokana na mwamuzi kutokuona kilichotokea.


Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 31 hakuisaidia timu yake kuepukika na kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Jaguares.

lundi 17 octobre 2022

Kuna Wachezaji mashoga EPL

Mwanasoka wa zamani wa England ambaye kwa sasa ni Mtangazaji wa michezo Gary Lineker (61), amedai kuwa anawajua wachezaji wawili wa Ligi ya England ambao ni mashoga na anatumani kuwa watajitokeza hivi karibuni.


”Huu ndio wakati mwafaka, wakati tunakaribia Kombe la Dunia,mjitokeze mtetee msimamo wenu ”

Akizungumza na gazeti la Daily Mirrow, Lineker alisema “Ninajua kwa uhakika kabisa kuwa hawa watu walikuwa karibu sana kujitokeza, ninawajua ni wapenzi wawili, lakini siwezi kuwataja,”

”Hofu ya Mashabiki na ukosoaji kutoka kwa wachezaji wenzao ndio unawafanya wengi wajifiche, na kubaki wakiishi maisha ya uwongo,”

”Ninajua ni ngumu sana, lakini nilikuwa natamani mjitokeze tu, sababu najua mpo, ni dhahiri kuna wachezaji wengi ambao wanalazimika kuishi kwa uwongo.”

Kombe la Dunia litafanyika mwezi ujao nchini Qatar ambako kutokana na sheria kali za Kiislamu mahusiano ya jinsia moja hayakubaliki na hukumu yake ni kifo.

samedi 8 octobre 2022

Type C lazima Ulaya

Moja kati ya habari kubwa Wiki hii ni hii ya Bunge la Ulaya kupitisha sheria mpya ambazo zitaanzishwa katika nchi za Umoja wa Ulaya, ambazo zinawalazimu Watumiaji na Watengenezaji wa vifaa vyote kama vile smart phones, vishkwambi, camera nk kutumia charger aina ya type c ifikapo mwaka 2024, hili likiwa ni jambo la kwanza duniani ambalo linatarajia kumuathiri Mtengenezaji wa simu za iPhone na Apple zaidi ya Wapinzani wake.


Kura hiyo inathibitisha makubaliano ya awali kati ya Taasisi za Umoja wa Ulaya kuifanya USB aina ya C inayotumiwa na vifaa vinavyotumia Android kuwa kiwango pekee cha Umoja wa Ulaya na hivyo kuilazimu Kampuni kutokea nchini Marekani Apple (AAPL.O) kubadilisha sehemu zake za kuchajia simu za iPhone na vifaa vingine.




Wachambuzi pia wanatarajia matokeo chanya kwa sababu inaweza kuwahimiza Watu kununua vifaa vilivyotolewa hivi karibuni vya kampuni hiyo, badala ya vile visivyo na USB-C.



Makubaliano haya pia yataathiri vifaa vya kusomea, na teknolojia nyinginezo, kumaanisha kuwa huenda pia mabadiliko hayo yakaathiri kampuni ya Samsung pamoja na Huawei.

mardi 20 septembre 2022

Nchi Kumi Ambazo ni Vigumu kwa Mwanaume Kupata Mwanamke wa Kumuoa

JAPOKUWA inafahamika kwamba, katika jumla ya idadi ya watu bilioni 7. 5 waliopo dunia leo hii, idadi ya wanaume na wanawake inapishana kwa kiasi kidogo, zipo baadhi ya nchi ambazo wanaume ni wengi kuliko wanawake, kiasi kwamba inakuwa kazi ngumu kwelikweli kumpata mwanamke wa kuoa.


JAPOKUWA inafahamika kwamba, katika jumla ya idadi ya watu bilioni 7. 5 waliopo dunia leo hii, idadi ya wanaume na wanawake inapishana kwa kiasi kidogo, zipo baadhi ya nchi ambazo wanaume ni wengi kuliko wanawake, kiasi kwamba inakuwa kazi ngumu kwelikweli kumpata mwanamke wa kuoa.


10.SWEDEN


Nchini Sweden, inaelezwa kwamba idadi ya wanaume, inazidi kwa 12,000 zaidi ya idadi ya wanawake waliopo na kundi kubwa ni la vijana. Idadi hii inatarajiwa kuongezeka zaidi kwa hiyo, wanaume wengi wanajikuta katika wakati mgumu wa kupata wachumba wa kuingia nao kwenye ndoa.

Sababu nyingine inatajwa kwamba ni ongezeko la wahamiaji kutoka kwenye nchi zenye vita ambao wanapata hifadhi kwenye nchi hiyo na baadaye kupewa uraia. Ongezeko la wahamiaji, limesababisha wananchi wengi wa Sweden wasiotaka shida, kuhamia kwenye nchi nyingine zisizo na idadi kubwa ya wahamiaji na wengi wanaoondoka, ni wasichana.

9.AFGHANISTAN


Kabla ya nchi ya Afghanstan kukumbwa na vita, ilikuwa ikisifika kwa kuwa na wanawake wengi warembo waliokuwa wakionekana kwa wingi mitaani, hasa katika Jiji la Kabul.

Hata hivyo, tangu machafuko yaikumbe nchi hiyo, idadi ya wanawake imepungua sana, sababu kubwa ni kwamba wanawake wengi na watoto wameikimbia nchi kutokana na vita na kwenda kutafuta hifadhi katika nchi zenye usalama. Waliobaki ni wanaume wanaoendelea kupambana na machafuko ya mara kwa mara yanayoibuka na kupotea, matokeo yake imekuwa vigumu sana kupata mke wa kuoa.

8.NIGERIA


Nchini Nigeria, uwiano kati ya wanawake na wanaume, haupo sawa. Wanaume ni wengi kuliko wanawake na sababu kubwa, inatajwa kwamba wanawake wa Kinigeria, wamekuwa wakiikimbia nchi yao na kwenda kutafuta hifadhi kwenye mataifa mengine kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo kukimbia ndoa za utotoni, tohara za wanawake na hali ngumu ya kimaisha.

Hivi karibuni, serikali ya nchi hiyo ilieleza kuhusu tatizo la vijana wengi waliofikia umri wa kuoa, kukosa wanawake wa kuwaoa.

7.UGIRIKI


Kwa kipindi kirefu, nchi ya Ugiriki ilikuwa ikitumika kama kituo cha watu wanaotoka Ulaya, hasa katika nchi za Uingereza na Ufaransa kwenda kwenye mabara mengine. Kutokanana uzuri wa hali ya hewa ya Ugiriki pamoja na mandhari yake, wasafiri wengi wakawa wanavutiwa kuendelea kukaa kwenye nchi hiyo na baadaye, idadi ya wahamiaji kutoka kwenye mataifa makubwa ya Ulaya iliongezeka na wengi kati yao, walikuwa ni wanaume.

Hali imeendelea hivyo kwa miaka mingi na kusababisha idadi ya wanawake kutotosheleza idadi ya wanaume wanaozidi kuongezeka kila kukicha. Hivi sasa ni vigumu sana kupata mke wa kuoa nchini Ugiriki.


6.MISRI


Misri ni moja ya nchi yenye idadi kubwa ya watu kwenye nchi za Kiarabu na barani Afrika. Kama zilivyo nchi nyingine za Kiarabu, wanawake wanatakiwa kufanya shughuli za nyumbani tu na kutoonekana hovyo mitaani.

Wengi wameitumia fursa hii kujiendelea kielimu wakiwa majumbani na wanawake wengi wa Misri, ni wasomi wenye digrii kadhaa, walizozipata kwa kujiendeleza wakiwa majumbani mwao na baadaye kwenda vyuo vikuu.

Hali hiyo imesababisha wanawake wengi wasomi, kuanza kutafuta ajira nje ya nchi, ambako wanawake wana uhuru zaidi na tayari wengi wameondoka na kwenda kufanya kazi mbalimbali kulingana na elimu zao, hali iliyosababisha wanaume wengi wapate kazi kwelikweli wanaposaka wanawake wa kuwaoa.

 
5.CHINA


China ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko wote duniani, lakini katika idadi ya watu wote nchini humo, wanaume wanawazidi wanawake kwa idadi ya watu milioni 40. Tofauti hii kubwa kati ya idadi ya wanawake na wanaume, imesababishwa na Wachina kuwa na kawaida ya kuchagua watoto, na mwanamke anapokuwa na ujauzito wa mtoto wa kike, hulazimishwa kutoa ujauzito huo kwani Wachina wengi wanaamini kwamba mtoto wa kiume ndiyo mwenye thamani katika jamii.

Hali hiyo imesababisha uhaba mkubwa wa wanawake mitaani, kiasi cha serikali kuingilia kati na sasa, vijana wa kiume kutoka China wanaruhusiwa kwenda kutafuta wanawake nchini Urusi, ambako kuna uhaba wa wanaume.

4.MAREKANI


Yawezekana ukashangazwa na kusikia kwamba nchini Marekani nako kuna uhaba mkubwa wa wanawake. Ukweli ni kwamba, katika baadhi ya majimbo, idadi ya wanawake ni ndogo kuliko wanaume.

Kwa mfano, katika majiji ya Los Angeles na Las Vegas, idadi ya wanawake ni ndogo kuliko wanaume kwa wastani wa wanaume 157 kwa wanawake 151, hali inayofanya iwe vigumu kupata wasichana wazuri wa kuoa.

 
3.INDIA


India ni miongoni mwa nchi zenye watu wengi zaidi duniani na inatarajiwa kwamba ifikapo 2024, itaizidi China. Licha ya idadi hiyo kubwa ya watu, India ina uhaba mkubwa wa wanawake kutokana na mila potofu ya nchi hiyo kwamba watoto wa kiume wana umuhimu sana kuliko wa kike wakiamini kwamba wana msaada mkubwa sana katika familia pale wanapofikia umri wa kujitegemea.

Wanaume wanawazidi wanawake kwa idadi ya watu milioni 37, hali inayofanya iwe vigumu sana kupata mke wa kuoa.


2.FALME ZA KIARABU


Katika kipindi cha karne ya 20 falme za kiarabu zilikuwa na idadi ya watu 40,000 tu, Kati ya hao wanawake wakiwa ni 22,000.Hata hivyo ugunduzi wa mafuta umesababisha nchi hiyo ibadilike haraka na wahamiaji wengi kutoka nchi mbalimbali,wengi wakiwa ni wanaume ambao wamejazana nchini humo,kutafuta maisha.

Hali hiyo imesababisha kuwe na uhaba mkubwa wa wanawake jambo linalowapa shida wanaume wanapofikia umri wa kuoa.

 
1.QATAR


Nchi ya Qatar ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa wa mafuta lakini kijiografia ina eneo dogo na wananchi wazawa wachache. Hata hivyo kutokana na utajiri wa mafuta imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo, hali ambayo imesababisha wahamiaji wengi kukimbilia na kutafuta maisha.

Matokeo yake wanaume wamekuwa wengi kwa wastani wa 3:1, katika kila watu wa 4 wa 3 ni wanaume na mmoja ni mwanamke na kuifanya kuwa nchi yenye wanawake wachache zaidi duniani.

dimanche 18 septembre 2022

Cardi B ahukumiwa siku 15

Cardi B amekiri makosa mawili yaliyotokana na ugomvi katika klabu ya utupu, kama sehemu ya makubaliano ambayo yanamaanisha kuwa ataepuka kesi na kufungwa jela.


Rapa huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy, mzaliwa wa Belcalis Almanzar, alikiri kosa la shambulio la kiwango cha tatu na kusababisha hatari kiwango cha daraja la pili, na alihukumiwa kifungo cha siku 15 katika huduma ya jamii.


Mashtaka mengine kumi yalitupiliwa mbali.

‘’Nimefanya maamuzi mabaya katika siku zangu zilizopita ambayo siogopi kukabiliana nayo na kuyasimamia,’’ alisema katika taarifa.

Mahakamani, kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 alikiri kuandaa na kushiriki katika mashambulizi mawili dhidi ya wafanyakazi wa klabu ya usiku ya Angels huko New York mnamo 2018.

Kulingana na mamlaka, matukio hayo yalikua ya ugomvi kati ya Almanzar na dada wawili - mmoja wao aliamini alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe, rapa Offset.

jeudi 8 septembre 2022

Malkia Elizabeth II ameaga dunia, Buckingham Palace imetangaza

Malkia Elizabeth II, malkia aliyehudumu muda mrefu zaidi nchini Uingereza, amefariki akiwa Balmoral akiwa na umri wa miaka 96, baada ya kutawala kwa miaka 70.


Familia yake ilikusanyika katika kasri yake ya Uskoti baada ya wasiwasi kuongezeka juu ya afya yake mapema Alhamisi.


mercredi 27 juillet 2022

Je kwenye Movie watu hufanya mapenzi kweli ?

Watu wengi huwa wanajiuliza kwamba zile scene ambazo katika Filamu za nje tunaona watu wakifanya mapenzi, je huwa wanafanya kweli au sio kweli.


Jibu ni kwamba mbali na PORNOGRAPHY Hakuna Filamu ambayo waigizaji wanafanya mapenzi kweli. Ninaposema kufanya mapenzi ninamaanisha Kugusanisha Sehemu za Siri, achana na mabusu na kushikanashikana.


Kinachofanyika kwenye hizo filamu ni kwamba scene ambayo inahitaji watu wafanye mapenzi kweli, au Scene inayohitaji kuonesha Sehemu za Siri za muigizaji kwa mfano Matiti, n.k basi watatafutwa Professional Porn Actors, kwa lugha ya filamu wanatambulika kama (Body Doubles) watatafutwa kisha watafanya yao kisha Kwa Techonology ya CGI (Computer Generated Images) zitapachikwa sura halisi za waigizaji.


Hivyo hivyo unaweza ukajiuliza mbona filamu fulani Star ameonekana Maziwa wazi, mfano Angelina Jolie kuna filamu yake moja yupo kifua wazi sana, huyo sio yeye ni ujanja tu wa Computer na matumizi ya Body Doubles.

lundi 18 juillet 2022

Mjomba wa Davido kuchaguliwa kuwa Gavana

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria mkali wa Afrobeats David Adedeji Adeleke alimaarufu kama Davido ameeleza furaha yake baada ya mjomba wake, Seneta Ademola Adeleke, kuchaguliwa kama gavana ajaye wa jimbo la Ogun katika awamu ya pili ya kuwania kiti hicho.
0
Seneta Adeleke alishinda kiti hicho kwa tiketi ya chala cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP).

Davido alikuwa mtu maarufu katika kampeni zake zote mbilimwaka 2018 na 2022 za kuwania kiti hicho.


"Familia ni kila kitu kwangu. Kando na hilo, sisi ni watu bora kwa kazi – tupatie mwaka mmoja au miwili na utaona nini kinatakachofanyika," nyota wa muziki aliiambia BBC Idhaa ya Pidginb kutoka mji wa kwa owa Ede kusini mwa Nigeria.

Rais Muhammadu Buhari alimpongeza Senator Adelekekwa ushindi wake, akisema kuwa "watu wa Osun wameelezea utashi wao kwa njia ya kura ".

dimanche 17 juillet 2022

Riyad Mahrez na sim yake iliyo haribika

Winga huyo wa klabu ya Manchester City ambaye kwa sasa analipwa kwa euro mil 120,000 sawa na Tsh 281,954,557/= kwa wiki Riyad Mahrez ametania kuwa hangeweza kumudu kutengeneza simu yake iliyoharibika hadi asaini mkataba mpya Manchester City.


Winga huyo wa Algeria ameongeza muda wa kukaa Etihad hadi 2025, baada ya kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa awali mwanzoni mwa mwezi huu.

Baada ya kukubali kufanyiwa marekebisho ya mkataba alikibali kusaini na alikuwa sehemu ya kikosi cha City kilichoondoka Jumamosi asubuhi kuelekea Marekani kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya.


wakati waondoka kuelkea Marekani Mahrez Alipost picha kwenye Twitter akiingia kwenye ndege, lakini wafuasi waligundua haraka kuwa alikuwa ameshika simu iliyopasuka.


'Mahrez una pesa,' shabiki mmoja alijibu, huku wengine wengi wakishangaa kwamba mchezaji wa Ligi ya Premia anaonekana kushindwa kurekebisha simu yake.

Lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 alitoa jibu la kufurahisha. "Nilikuwa nikisubiri mkataba mpya," alitania.

Mahrez alijiunga na City kutoka Leicester kwa pauni milioni 60 mwaka 2018 na amefunga mabao 63 katika mechi 189 alizochezea klabu hiyo.


Ameshinda Ligi ya Premia mara tatu chini ya uongozi wa Pep Guardiola - akiongeza taji moja alilonyanyua akiwa na Foxes msimu wa 2015-16 - na pia ameshinda Vikombe vitatu vya Carabao na Kombe moja la FA.