Google tag

lundi 18 juillet 2022

Mjomba wa Davido kuchaguliwa kuwa Gavana

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria mkali wa Afrobeats David Adedeji Adeleke alimaarufu kama Davido ameeleza furaha yake baada ya mjomba wake, Seneta Ademola Adeleke, kuchaguliwa kama gavana ajaye wa jimbo la Ogun katika awamu ya pili ya kuwania kiti hicho.
0
Seneta Adeleke alishinda kiti hicho kwa tiketi ya chala cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP).

Davido alikuwa mtu maarufu katika kampeni zake zote mbilimwaka 2018 na 2022 za kuwania kiti hicho.


"Familia ni kila kitu kwangu. Kando na hilo, sisi ni watu bora kwa kazi – tupatie mwaka mmoja au miwili na utaona nini kinatakachofanyika," nyota wa muziki aliiambia BBC Idhaa ya Pidginb kutoka mji wa kwa owa Ede kusini mwa Nigeria.

Rais Muhammadu Buhari alimpongeza Senator Adelekekwa ushindi wake, akisema kuwa "watu wa Osun wameelezea utashi wao kwa njia ya kura ".

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire