Google tag

mercredi 27 juillet 2022

Je kwenye Movie watu hufanya mapenzi kweli ?

Watu wengi huwa wanajiuliza kwamba zile scene ambazo katika Filamu za nje tunaona watu wakifanya mapenzi, je huwa wanafanya kweli au sio kweli.


Jibu ni kwamba mbali na PORNOGRAPHY Hakuna Filamu ambayo waigizaji wanafanya mapenzi kweli. Ninaposema kufanya mapenzi ninamaanisha Kugusanisha Sehemu za Siri, achana na mabusu na kushikanashikana.


Kinachofanyika kwenye hizo filamu ni kwamba scene ambayo inahitaji watu wafanye mapenzi kweli, au Scene inayohitaji kuonesha Sehemu za Siri za muigizaji kwa mfano Matiti, n.k basi watatafutwa Professional Porn Actors, kwa lugha ya filamu wanatambulika kama (Body Doubles) watatafutwa kisha watafanya yao kisha Kwa Techonology ya CGI (Computer Generated Images) zitapachikwa sura halisi za waigizaji.


Hivyo hivyo unaweza ukajiuliza mbona filamu fulani Star ameonekana Maziwa wazi, mfano Angelina Jolie kuna filamu yake moja yupo kifua wazi sana, huyo sio yeye ni ujanja tu wa Computer na matumizi ya Body Doubles.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire