Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu hiyo
imesitisha kwa muda mazungumzo kuhusu mikataba ya Alexis Sanchez na
Mesut Ozil hadi mwisho wa msimu.
Sanchez na Ozil mikataba yao katika klabu ya Arsenal inamalizika mwezi juni mwakani na wamekuwa wakisusua kusaini mikataba mipya ya kuendelea kuitumika timu hiyo.
Mfaransa huyo amesema hayo wakati akihojiwa na kituo cha BeiN Sports huku akikataa kuweka wazi mustabali wake klabuni hapo.
Arsenal wameshuka hadi nambari sita Ligi ya Premia baada ya kushindwa mechi nne kati ya tano walizocheza karibuni zaidi.
Kuhusu mustakabali wake, Wenger alisema: “Bila kujali nitasalia katika klabu hii muda gani bado nitabaki kujitolea na kuangazia kabisa (majukumu yangu) muda wote nitakaokuwa katika klabu hii.”
Gunners watarejea uwanjani Ligi ya Premia Jumapili tarehe 2 Aprili watakapokuwa wenyeji wa Manchester City.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire