Geisson Perea akiwa sehemu ya ukuta wa mabeki kuzuia mpira wa adhabu (free-kick) uliyokuwa sehemu ya hatari zaidi karibu na lango la goli lao, aliamua kutoa nje sehemu zake za siri ili kumchanganya mpigaji wa mpira bila mwamuzi kuona tukio hilo lililonaswa na kamera za uwanjani.
Kitendo hiko kimetafsiriwa kama njia ya kumchanganya mpigaji wa mpira huo uliyokuwa umetengwa na mwamuzi kuelekea katika milingoti mitatu ya timu yake.
Kupitia Win Sports TV, Geisson Perea amesema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuiweka sawa bukta yake na sio kujiweka hadharani kwa ulimwengu. Hakufahamu pia kuwa kamera zilikuwa zikimmulika yeye.
Kwa mujibu wa Dailymail mashabiki wametaka mchezaji huyo apatiwe adhabu kali kutokana na kitendo hicho ambacho ndani ya uwanja hakupatiwa kutokana na mwamuzi kutokuona kilichotokea.
Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 31 hakuisaidia timu yake kuepukika na kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Jaguares.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire