Google tag

mercredi 23 novembre 2022

Timu za Taifa za England na Wales zimetangaza kuwa manahodha wao hawatovaa vitambaa vilivyoandikwa "OneLove"

Timu za Taifa za England na Wales zimetangaza kuwa manahodha wao hawatovaa vitambaa vilivyoandikwa "One Love" baada ya kupewa taarifa kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kupewa kadi ya njano mara tu watakapo ingia uwanjani.

Taarifa ya pamoja kutoka kwa Mashirikisho ya soka ya England 🇬🇧 , Wales ,Belgium 🇧🇪 ,Denmark 🇩🇰 ,Germany 🇩🇪 , Netherlands 🇳🇱 na Suisse 🇨🇭 imesema kuwa.. 






"FIFA imeweka wazi kabisa kuwa itatuwekea vikwazo vya kimichezo ikiwa manahodha wetu watavaa vitambaa hivyo uwanjani"

"Sisi kama Mashirikisho, hatuwezi kuacha wachezaji wetu wawekewe vikwazo,hivyo tumewaarifu Manahodha wasifanye hivyo katika mechi yoyote ya Kombe la Dunia"


"Tumechanganyikiwa na uamuzi huu wa FIFA ambao haujawahi kutokea, tuliwaandikia barua mwezi Septemba kuomba ruhusa ya kuvaa vitambaa hivi lakini hatukujibiwa."


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire