1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye
kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke
akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa
amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea
nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye
tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza.
Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa
kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani
huwezi kazi kabisa!”
2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la
ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na
watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea
kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo,
hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu
mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni
wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale
wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu
kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya
mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali
amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja
kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.”
Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
3:USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya
upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na
kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa
mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa.
Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.
4:GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za
kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala
miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha
ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza
kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi
unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume
zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao
hao.
5:USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata
tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au
kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye
humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.
Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire