Alibaba

mercredi 15 mai 2013

Wapenzi Washitakiwa Kwa Kukaa Uchi Ufukweni

Wapenzi wamekamatwa katika ufukwe wa South Carolina baada ya polisi kuwabamba wakiwa hawajavaa nguo na mmojawao ‘akiwa amelewa kupindukia
Jasmine Kim Walton, miaka 21, na Kyle Martin Schnoebelen, miaka 22, wote kutoka Virginia walikamatwa muda mfupi kabla ya kufikia Saa 9 alfajiri ya Jumapili.

Waliwaeleza polisi kwamba walikuwa wamekwenda kuogelea kwa kupiga mbizi na waliporejea wakakuta nguo

WEMA BWANA!

Joseph Shaluwa na Hamida Hassan
HATA kama ukimkwepa vipi, lazima utakutana na stori yake tu! Staa wa Bongo, Wema Sepetu anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine, safari hii ametokelezea na mwanaume mwingine katika pozi tata lililozua minong’ono kwa mashabiki wake.
Wema akiwa katika pozi la kimahaba na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Raheem.
Wema ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, huku akifurukuta kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ametokelezea na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Raheem katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
GUMZO MITANDAONI
Picha hiyo ambayo pozi lake ni ‘very romantic’ imezua gumzo katika mitandao mbalimbali ilipotundikwa na wadau wengi walionekana kuamini kuwa Wema alikuwa akimnadi mpenzi wake mpya.
Mtoa maoni mmoja aliandika: “Naona Wema ameamua kutuonesha shem wetu mpya, sasa hapo kazi kwa wenye vijicho.”
Mwingine aliandika: “Mmh! Mbona (Raheem) haonekani uso? Kama lengo lake lilikuwa kumwanika angemuacha tu aonekane ila dah! Ana kifua kizuri sana. Huyu jamaa anaonekana anafanya sana mazoezi.”
DIAMOND ATAJWA
Katika gumzo hilo, wengine walikwenda mbali zaidi, wakisema kwamba inawezekana Wema alikuwa na Raheem kwa siri muda mrefu lakini sasa ameamua kuvunja ukimya ili kumringishia x - boyfriend wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Siku zote alikuwa wapi? Atakuwa anamwoneshea Diamond tu huyu,” mtoa maoni mwingine aliandika.
INTERVIEW NA RAHEEM
Ni jadi ya magazeti ya Global Publishers likiwemo hili la Risasi Mchanganyiko kutafuta mzani wa habari kabla ya kwenda hewani hivyo lilimtafuta Raheem ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha.
Raheem alikiri kuitambua picha yake na Wema lakini alisema imemshtua na kumcha-nganya maana hakutegemea kama ingefika mitandaoni na hatimaye kwenye vyombo vya habari.
Wema Sepetu.
Alisema: “Ni kweli nilipiga hiyo picha na Wema lakini ni ya kawaida tu, haina maana nyingine tofauti. Wema ni rafiki yangu na dada yangu. Tunaheshimiana, hakuna cha zaidi.
“Wema ni maarufu na watu wanaweza kujaji wanavyotaka, hilo litanisababishia matatizo kwa sababu mimi nina mpenzi wangu na Wema si mtu wangu kabisa...she is just my sister (ni dada yangu tu).”
Risasi: Hiyo picha mlipiga lini, wapi na kwa matumizi gani?
Raheem: Ilikuwa kwenye function (tukio) fulani ambayo siwezi kuizungumzia. Kama wiki sita au miezi miwili hivi iliyopita na tulipiga kama marafiki tu, hakuna cha zaidi.
Risasi: Kwa hiyo Wema akithibitisha wewe ni mpenzi wake itakuwaje?
Raheem: Nitamshangaa sana! Wema ni dada yangu tu.
Risasi: Inasemekana Wema ameamua kuianika hiyo picha kwa lengo la kumrusha roho Diamond, unasemaje hapo?
Raheem: Sijui na kwa kweli siwezi kuzungumzia mambo ya mtu binafsi. Sijui chochote.
GONGA HAPA KUMSIKIA WEMA
Wema alipatikana na kusomewa mashitaka yake ambapo alikiri kupiga picha na Raheem, akafafanua kuwa aliipiga muda mfupi baada ya kutoka kufanya interview na kituo kimoja cha redio (jina kapuni) lakini akasema haina uhusiano wowote na suala la mapenzi.
“Ni kweli nilipiga hiyo picha, yeye aliniomba tu kama fan (shabiki) wangu, akataka ku-show love (kuonesha upendo), sikuona sababu ya kumkatalia. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Martin (Kadinda – meneja wake) na baada ya siku hiyo sijawahi kuonana naye tena mahali popote...sioni tatizo kabisa, ni kawaida kwa sisi mastaa,” alisema Wema.
Risasi: Lakini Wema wadau wanasema eti ni mpenzi wako na umefanya hivyo kwa lengo la kumrusha roho Diamond.
Wema: Umeshasema wadau, waache na mambo yao lakini maelezo yangu ni hayo na naamini yamejitosheleza.
Risasi: Kuna kitu nahitaji ufafanue zaidi...lile pozi lipo romantic sana, hufikiri kuwa inaweza kuwa sababu ya watu kuwa na hisia kwamba ni mpenzi wako?
Wema: Ni kweli picha ni romantic lakini yule kijana (Raheem) si mpenzi wangu. Naomba nieleweke hivyo. Ahsante.

DIAMOND, NEY WAMITEGO KUZINDUA VIDEO YA MUZIKI GANI' NDANI YA DAR LIVE MEI 18, 2013


11 KORTINI KWA KUZINI NA MBWA

WANAWAKE 11 raia wa Kenya pamoja na Mzungu raia wa Sweden, hivi karibuni wamefikishwa katika mahakama moja iliyopo Mombasa kwa kudaiwa kunaswa wakirekodi mkanda wa ngono na mbwa.
Wanawake hao waliotajwa kwa majina ya Beatrice Mueni Mwosa, Waithera Karanja, Marry Nyambura Kimani, Magdaline Wairimu, Celestine Nekesa, Dorcus Melisa, Ludia Nyaboke, Phidelia Mawia, Anne Wanjiku, Cecilia Nzambi na wengineo wanadaiwa kunaswa na polisi katika eneo la Nyali wakifanya uchafu huo.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa katika eneo hilo, ilikutwa kamera na kompyuta mpakato ‘laptop’ mali ya Mzungu huyo anayedaiwa kuratibu mpango mzima, vitu ambavyo vilichukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Katika hatua nyingine, imedaiwa kuwa mwanaume huyo Msweden aliingia nchini humo kama mtalii na akawa karibu sana na mwanamke Mkenya ambaye inadaiwa ndiye aliyewakusanya wanawake wengine kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.
Hata hivyo, upande wa mashitaka utakuwa na kazi kubwa ya kuthibitisha kama kweli wanawake hao wamehusika kwani inadaiwa wakati wanakamatwa, mmoja tu ndiye aliyekuwa amesharekodi ‘scene’ yake.
SERIKALI YA KENYA YACHARUKA
Wakati kesi ikiendelea mahakamani, makamu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto ameeleza kusikitishwa na tukio hilo, akasema amewaagiza watu wa usalama kuhakikisha raia wa kigeni wenye tabia chafu kama hizo wanatimuliwa mara moja.
“Nimewaambia watu wa Internal Security (Usalama wa Ndani) kwamba watu kama hawa hawafai kuwa katika taifa letu la Kenya, wapandishwe ndege waende kwao,” alisema Ruto.
WABONGO WAONYWA
Kufuatia tukio hilo, mademu Bongo wenye uhusiano wa kimapenzi na Wazungu wametakiwa kuwa makini kwani baadhi si watu wema.
Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko baada ya kesi hiyo kuwa gumzo, baadhi ya watu wamesema kilichotokea Kenya ni fundisho kwa wasichana wa Kibongo wanaoshobokea Wazungu.
“Hilo limetokea Kenya lakini ni fundisho kwa mabinti wetu hapa nchini ambao wanakimbilia kuanzisha uhusiano na Wazungu.
“Kuna uwezakano wapo wanaofanyiwa vitendo hivyo kwa kuahidiwa pesa nyingi au kuwekewa mitego na hatimaye kurekodiwa picha chafu wakiwa wanajua au hawajui,” alisema mama Salma wa Magomeni jijini Dar aliyedai kwamba amekuwa akifuatilia kesi hiyo tangu ilipoanza kusikilizwa.