Google tag

samedi 28 décembre 2013

swahili love sms


Uzuri wa usiku si giza lifunikalo dunia wala si kimya kinachotawala mazingira bali ni njozi njema zenye maono na matarajio yenye mafanikio. Nakutakia ucku mwema
*°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Naituma  sauti yangu"" izunguke"" moyo"" wako kwa""upendo"" iuguse"" uso"" wako""kwa"" busu""na"" mwisho""ikunong'oneze"" sikioni"" taratiiiiibu"" Gd9t
    *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
mpnz wangu ninavyo jua mm huwezi kutupa mawe kwenye mti usiokuwa na matunda mazuri maana hivyo basi tambua ww ni mrembo xanandani ya moyo wangu usiniache pekeyangu kwani na kupenda xana tabua hilo mpnz wangu
      *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Niseme nini ujue nakupenda? Nifanye nini ujue nakupenda? Nikuite jina gani ujue ni wewe peke yako upo moyoni mwangu? Hakika hakuna ila moyo wangu ndio naosema kuwa nakupenda, niamini mpenzi!
       *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
nina mambo saba ya kukuambia ,lakini kwa sasa nakumbuka 6tu,bila shaka matano ndio muhimu kwa leo ,ila unayopaswa kujua ni manne kwa sasa ,oooh usijali nitakuambia ma3 tu,ila kwa jinsi ulivyo naona nianze na ma2 muhimu,ila yatakugusa sana na kwa kuwa sipendi kukuumiza naomba niseme moja tu .mchana mwema dia
       *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
kwa hakika inzi hufia kidondoni,shujaa vitani ,mtaliii mbugani ,je mwenye penzi la dhati hufia kwa ampendaye?
       *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
upendo sio tigo eti ongea kwa nusu shilingi wala sio voda kazi ni kwako, pia sio airtel jisikie huru bali upendo ni zawadi pekee sana mungu aliyoiweka ndani ya mioyo yetu.hili ni la kuzingatia dear nakupenda sana
      *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
yakumbuke haya sana katika maisha yako wahurumie wenye kukupenda hasa mwenye pendo la dhati kama langu,wapende wanaokupenda japo kwa chembe ya upendo,thamini pendo la akupendae kwa kila mara japo sekunde moja.     
       *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
nalia ukiwa mbali, nachukia nisipo kuona ,najuta ninapo kuudhi ,naumia unapo nitenga , nateseka ukiwa kimya ,nafurahi ukinikumbuka, nakupnda mpz
   ●´¯`´¯`●♥¡¡♥●´¯`´¯`●♥
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifan
 *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
nimegundua dawa ya maisha ukinichukia nakupenda,ukiniudhi nakufurahisha,ukinisahau nakukumbuka,ukikaa kimya nakusalimia,na ukinisahau kuniombea kwa ALLAH nitakukumbusha.
          *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°
najua mimi sio wa kwanza kukuombea mema ,ila napenda kuwa ni mmoja kati ya  wanaokutakia asubuhi njema.
           *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°

unaweza ukafunga macho kwa usilolitaka kuliona lakini hauwez kufunga moyo wako kwa Unalo Lipenda. Nakupenda Mpenzi

        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
upepo wangu wakupuliza wewe kutokana na joto kali usijaribu kwa kuvaa sweta ukapunguza ukali ninachotaka mi nikuwa na wewe naomb unielewe .
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Uzuni ,upole,ukarimu wanakusalimia. Furahana unyenyekevu wapo njiani wanakujakwako .ila taabu nashida hawatakuja kwasababu wote wanaumwa.mawazo mashakana kukata tamaa wapo jela.ushindi utajiri na amani wapo njiani wanakuja gday
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
 rafiki mwaminifu ni mlinzi mahiri na aliyempata amepata hazina isiyokuwa na kifani,ahsante kwa kuwa rafiki mwaminifu.
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
     usiku huu tulivu nikiwa nimejilaza kitandani natamani nisikie sauti yako ambayo hunikosha na kunikosesha raha nisipoisikia.uwembamba Wa Sauti Yako Hupenya Kwenye Ngoma Ya Masikio Yangu Hunitekenya Na Kuniacha Nikifurahi. Nakupend Wangu Kipenzi
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
   maumivu ya kulipoteza penzi lako ni kubwa,lakini ni makubwa zaidi baada ya kugundua haukuwa yule nileyedhani. inaniuma sana
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
     maneno million  haliwez kulirudisha pendo lako najua kwasababu nimejaribu,pia machozi million haliwez kulirudisha najua kwasababu nimelia.
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Kuna miezi 12 katika mwaka…siku 30 katika mwezi…siku 7 katika wiki, masaa 24 katika siku…dakika 60 katika saa……lakini wewe ni mmoja tu maishani mwangu.
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*

Kuna vitu viwili zinavyoniamsha asubuhi na mapema: Alamu ya saa yangu na wewe

        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo, suluhu na sababu; ubongo wa kisayansi huwa na kanuni, nadharia na takwimu; wangu una wewe tu!
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Penzi linaweza kuelezewa kwa namna nyingi. Namna moja niijuayo nikumtumia mapenzi hayo mtu asomaye meseji hii.
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako kuwa pamoja
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Umewekwa usiku ili tuweze tuukubali mchana, huzuni ili tuikubali furaha, ubaya ili tuukubali uzuri, wewe ili niyakunali mapenzi.
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Mapenzi ni nini? Wale wasiopenda huita majukumu, wale wanaoyachezea huita mchezo, wale wasiokuwa nayo huita ndoto, na wale wanaoelewa huyaita mwisho wa safari, na mimi, mwisho wangu ni wewe.
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Ni mapenzi gani yanayofanya simu yako ilie kila nitumapo meseji?
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Unaonekana kung’ara leo nilijuaje…….ni kwasababu unaonekana hivyo kila siku
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Kama mapenzi huweza kukimbiwa kwa kufumba macho yetu tu, basi nisingefunika macho kabisa. Sitaki sekunde ipite bila kukupenda wewe.
        *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli, lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe.
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe, kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Mwanamke ni yule amfanyaye mwanamme auhisi uanaume wake, wewe ni mwanamke mwenye sifa hizo.
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*
Kukusahau wewe ni ngumu lakini kunisahau mimi ni juu yako. Usinisahau kamwe, unaweza kuisahau meseji hii, lakini si mtumaji.
         *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*

DIAMOND, WEMA WATANGAZA NDOA

Stori: Shakoor Jongo na Imelda Mtema
HUKU mchumba’ke, Penniel Mungilwa ‘Penny’ akifungasha virago kurejea kwao, mzee mzima Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza kumuoa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’(kushoto) na Penniel Mungilwa ‘Penny’ wakiongea jambo enzi za mapenzi yao.
Ishu hiyo ilijiri ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar ambapo mkali huyo wa Bongo Fleva alikuwa akikamua kwenye sherehe ya Krismasi aliyoiandaa mwenyewe.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kupanda jukwaani katika viwanja vya leaders.
TANGAZO LA AWALI
Awali kabla ya kufikia eneo la kutangaza kuoana, Diamond aliweka wazi jukwaani kwamba yeye na Wema wamerudiana.
Diamond Platnumz akiongea jambo baada ya Wema Isaac Sepetu ‘Madam’  kupanda jukwaani.
MTIRIRIKO ULIVYOKUWA
Diamond, akiwa ameshika kipaza sauti alikatisha kuimba na kuwauliza mashabiki wake, hasa watoto waliohudhuria kwa wingi tamasha hilo, je, wanataka kumuona shemeji yao?
“Itakuwa si vizuri mkaondoka bila kumuona shemeji yenu, nikuleteeni mumuone?” aliuliza  Diamond. Swali hilohilo akalirudia tena ambapo lilipokelewa kwa shangwe huku mashabiki wakilitaja jina la Wema.
                                        Diamond Platnumz na Wema Isaac Sepetu wakijiachia.
WEMA APANDISHWA JUKWAANI
Kufuatia kelele za mashabiki, Diamond alimuomba Disco Joker (DJ) wake amuwekee Wimbo wa Ukimwona ambao ulisindikiza ujio wa Wema jukwaani akifuatana na wapambe wa Diamond.
“DJ acha huo, nipigie Wimbo wa Ukimwona watu wangu wa nguvu wamwone shemeji yao kwani tangu nilivyokwenda naye China walikuwa wakisumbuliwa na maneno tofautitofauti kutoka kwenye mitandao ya kijamii,” alisikika Diamond.
Diamond, akiwa ameshika kipaza sauti akiima Wimbo wa Ukimwona na Wema akiwa amemkumatia.
JUKWAA SASA
Hali haikuwa ya kawaida jukwaani kwani kilichofuata hapo ni Wema kuonesha kwa vitendo mambo yaliyoashiria kuwa, wawili hao sasa ni mwendo mdundo.
Wema alishuhudiwa akimzungushia mikono Diamond kwenye kiuno jambo ambalo liliwafanya baadhi ya mashabiki wa mastaa hao kutoa machozi ya furaha kuona penzi la wawili hao limerudi upya, wengine walimwambia Diamond amuoe Wema.
“Diamond muoe Wema, mnapendezana sana,” walisikika mashabiki.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’akimuaga Diamond Platnumz kwa kumkumatia.
MAWIFI WADAI KUHARIBIWA SIKU NA KAKA YAO
Hata hivyo, kitendo cha Diamond kumwita Wema jukwaani kilionekana kuharibu furaha ya sikukuu kwa ndugu zake kwani bila ya kuuma midomo dada zake staa huyo wakiongozwa na Esma Khan walinuna na kuanza kuondoka.
“Yaani siku yangu imeshaharibika, nilikuja nina furaha sasa imepotea, tuondokeni ndugu zanguni,” alisema Esma akiwaambia Mwanaisha Abdul ‘Queen Darleen’ na Halima Haroun ‘Kimwana’.

Diamond Platnumz na Penny wakiwa pamoja enzi za mapenzi yao.
MAMA DIAMOND ASHANGAA
Kitendo cha ndugu hao kukasirika hakikupokelewa vizuri na bi mkubwa wao yaani mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye aliwajia juu akiwashangaa.
“Wajinga nini? Sasa walitaka Diamond… (tusi) wao, mtu ameshaamua kupenda wamwache, mi’ mwenyewe nimeshajifunza, sitaki kuingilia penzi lake,” alisema mwanamke huyo ambaye mjini anazungukia usafiri aina ya Altezza.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’  na Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Baada ya shoo hiyo iliyomalizika saa moja usiku, paparazi wetu alimfuata Diamond akiwa amesimama na Wema na kuwauliza kama kweli wana nia ya kufunga ndoa.
“Hilo mwana mbona lipo wazi, nataka kumuoa staa na nataka kuzaa na staa,” alisema Diamond huku Wema akiwa hapingi.

MAMA WEMA ATANGAZA VITA  NA DIAMOND
Wakati Dimaond akitambia ndoa na Wema, siku hiyohiyo ya Krismasi, mama wa Wema, Mariam Sepetu alidaiwa kutangaza vita na mwanamuziki huyo baada ya kusikia tetesi kuwa amerudiana na mwanaye.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mama Wema (jina tunalo) mama wa staa huyo alichukizwa na kitendo cha Diamond kurudiana na mwanaye kwani anaamini anamchezea tu.
Mama wa Wema, Mariam Sepetu.
Rafiki huyo alizidi kudai kuwa, taarifa hizo zimemuweka  mama huyo kwenye wakati mgumu na kudai kuwa popote atakapokutana na mwanamziki huyo atampopoa mawe au machungwa hata ikiwa siku ya ndoa yao.
“Mama Wema amesema hampendi Diamond, popote atakapomuona itakuwa vita ya wawili, kama kuna jiwe atamrushia, hata machungwa kama yapo yatakuwa halali yake,” alisema rafiki huyo.

WOSIA WA MZEE SEPETU
Mpashaji huyo wetu alizidi kufunguka kuwa, mama Wema ana wosia mkononi ambao aliuacha marehemu mumewe, mzee Isaac Abraham Sepetu.
Alisema katika wosia huo, mzee huyo alisema hataki Diamond amuoe Wema na kama mrembo huyo atakiuka  wosia huo atapatwa na laana mbaya katika maisha yake.
“Kinachomuumiza zaidi mama Wema ni huo wosia, mzee Sepetu alisema hataki mtoto wake aolewe na Diamond, kama atakataa kuna kitu kibaya kitamkuta katika maisha yake,” alisema rafiki huyo.

MAMA WEMA ASAKWA
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimvutia waya mama Wema ili kuweza kuthibitisha madai hayo ambapo alisema kuwa, hayuko tayari kuzungumzia jambo hilo kwa wakati huo mpaka atapoamua akisisitiza muda si mrefu.
“Jamani nina mambo mengi sana ya kufanya na sijatulia kabisa siko tayari kuzungumza chochote kwa sasa nikiwa tayari nitawaambia kila kitu,” alisema mama Wema.