Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ akizungumza machache mbele ya watu waliohudhuria.
Jana ilikuwa ni siku ya furaha kwa wasanii
wa Kundi la Bongo Movie Unity waliokuwa wakisherehekea kundi hilo
kutimiza miaka mitatu tangu lilipoanzishwa.
Sherehe za kumbukumbu hiyo zilifanyika
kwenye Ukumbi wa Arcade, Mikocheni jijini Dar ambapo wasanii walianza
kwa kupiga picha kwenye zulia jekundu ‘red carpet’ na watu kibao
waliohudhuria.
Kwa upande wa burudani ya muziki,
wanamuziki Linex, Amini, Pendo wa Maisha Plus, Shilole, Bendi ya Fm
Academia na Bendi ya BM walitoa burudani ya aina yake na kusababisha
ukumbi wote kulipuka kwa shangwe.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire