Google tag

lundi 2 juin 2014

MAKAMUA: WAKALI KWANZA LIMEBAKI JINA TU

Makamua akihojiwa na Global TV Online.
MAKALA NA ANDREW CARLOS
WAKALI kwanza ni moja kati ya makundi ambayo yalitikisa sana katika muziki wa Bongo Fleva mwaka 2006-2009. Kundi hili lilibebwa na vichwa vyenye madini, Josline, Makamua na Q-Jay.
Mashabiki wengi walipenda nyimbo zao na miongoni mwa wimbo ambao ulitikisa sana ni pamoja na ule wa Natamani.
Makamua, mmoja kati ya vichwa vilivyokuwa vikiunda kundi hili juzikati alifanya mahojiano na Global TV Online, amewakumbushia vitu vingi, tujiunge naye:
Presenta wa Global TV Online, Erick Evarist akifanya mahojiano na Makamua.
ILIKUWAJE MKAUNDA WAKALI KWANZA?
Ni kama ‘oganaizesheni’ ambayo tuliianzisha  kwa kuona tunaweza kufanya hivyo kwa pamoja kama vijana sababu ya kuepuka vitu mbalimbali kupitia muziki.
Kundi lilianza nikiwa na Josline kipindi hicho alikuwa akitamba na wimbo wa Perfume aliorekodi katika Studio za Midman Records.
Mazoea ya kufika Studio za Midman ndiyo yalisababisha kukutana na Q-Jay, tukaona tunaweza kutengeneza kundi la pamoja.
Kulikuwa na majina tofauti ya kupendekeza kwa ajili ya kundi, mimi nikapendekeza jina la Wakali Kwanza likawa ‘lika-sound’ vizuri basi kila mtu akakubaliana nalo, tukalipitisha.
Mtu wa kwanza kusikiliza kazi zetu na kutukubali alikuwa ni Steven Mdoe ‘Dj Skillz’ akatukubali kinomanoma.
NGOMA GANI ILIWATAMBULISHA WAKALI KWANZA?
Tulianza kwa ‘project’ ya kila mtu kivyake. Nilianza kwa kurekodi wimbo wa Wanatamani kisha baadaye nikatoa wimbo wa Rudi Nyumbani nikimshirikisha Enika kipindi hicho Q-Jay alitoa wimbo wa Sifai, Josline alitoa Niite Basi na Mshikaji Mmoja.
Erick Evarist akizidi kulonga na Makamua.
Baadaye Josline alikuwa nje ya kundi lakini tuliendeleza love kwa kuwa naye kwenye wimbo wa Natamani.
Tukapotezana tena kila mmoja na mitikasi yake. Q-Jay akaingia kwenye nyimbo za Injili (akaokoka) Baada ya kimya kidogo nikatoka kivyangu na wimbo wa Don’t Cry nikimshirikisha  Sarah kutoka Sweden.
VIPI MNA MPANGO WA KURUDI TENA KAMA KUNDI?
Kutusikia wote watatu kwa kipindi hiki itakuwa ngumu. Kama nilivyokwambia Q-Jay ameokoka labda itokee nyimbo ya gospel ambayo itahamasisha watu wa dini ndio tunaweza kutoka watatu.
WEWE NA ENIKA MLIKUTANIA WAPI?
Mara ya kwanza tulikutana kwa marehemu Roy aliyekuwa studio za G records. Kwa sasa yupo anafanya sana adverts (matangazo) siwezi kueleza kwa nini labda kwake anapata benefit (faida) zaidi.
UNAMZUNGUMZIAJE DIAMOND NA TUZO ZA KILI?
Wanasema sometimes ukikaa nje ya mchezo unawea kuona mengi zaidi. Kwa maoni yangu naona kuwa amestahili kupata. Time imekuja vizuri kwake na ametumia muda vizuri na mchezo umeonekana kwenda vizuri kwake.
Joslin, Makamua wakipozi na Mwana hip hop, Kekuu.
Sema nimeona amekuwa katika category nyingi sana. Na kama mtu akichukua tuzo nyingi vile inaonekana kama watu hawajafanya kazi kabisa. Kuna watu kama Rich Mavoko, Ommy Dimpoz wamefanya kazi nzuri.
ULISHAWAHI KUSHIRIKI KWENYE TUZO ZOZOTE?
Mara ya kwanza kabisa nilitakiwa kuwa nomineted na sijui kwa nini sikuwekwa kwa sababu kipindi hicho nilitoa wimbo wa Rudi Nyumbani ambapo alichukuwa mwenzangu Q Jay lakini nikaona mzuka pia.
UNASHAURI KWA WAANDAAJI TUZO ZA KILI?
Kamati zikae chini na kucheki ‘countdown’ zote haijalishi ‘media’ ipi. Wajaribu pia kugawa category kutokana na ‘game’ ilivyotoka na wala sio kwa kukariri.
UKIMYA
Niko na nyimbo nyingi ila kwa sasa narudi na project yangu maalum. Nina wimbo unaitwa Nitakulinda nilioshirikiana na Josline nimeufanya Legendary Music pande za Kinondoni.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire