Kampuni ya Acer imezindua laptopu ya kwanza ilio na kioo kilichojipinda.Acer inasema kuwa uvumbuzi huo utaiwezesha kucheza michezo ya video.
Televisheni kadhaa pia zimetumia uvumbuzi huo,lakini umezua mgawanyiko kwa kuwa una umuhimu na ubaya wake.
Kampuni hiyo ya Taiwan pia ilitangaza kwamba imefanikiwa kupata tekenolojia ya pet katika mkutano na wanahabari mjini Berlin.
Kampuni kadhaa za kielektroniki ikiwemo Samsung,Lenovo,DJI,Sony na Huawei zinatarajiwa kuzindua sura mpya ya laptopu zake katika maonyesho ya kiteknolojia ya Ifa katika mji mkuu wa Ujerumani wiki hii.
Laptopu hiyo ina kioo kikubwa ikilinganishwa na laptopu ya kawaida ya Acer,lakini ni umbo lake ambalo liliifanya kampuni hiyo kudai kuwa ya kwanza kuzinduliwa duniani.
Google tag
vendredi 2 septembre 2016
Acer yazindua laptopu yenye kioo kilichojipinda
Inscription à :
Publier les commentaires (Atom)
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire