Alibaba

mardi 20 septembre 2016

Arsene Wenger amtolea mbov Pep

ARSENAL oya oya. Baada ya kuigonga nne Hull City huko kwenye vyumba vyao vya kubadilishia ni mwendo wa kupiga selfie tu, kisha Kocha wa Arsene Wenger akachimba mkwara labda Manchester City watibue mipango.

Arsenal imeshinda mechi tatu mfululizo za ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka huu uanze na tamu zaidi wamefunga mabao saba katika mechi zao mbili za karibuni walizocheza ugenini.

Hata hivyo, Wenger amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba wasifurahie sana kupita kiasi kwa sababu kuna timu moja inawapa homa, Manchester City ya Mhispaniola Pep Guardiola.

Man City wameiacha Arsenal kwa pointi tano kileleni kwenye msimamo na Wenger anasema: “Kwa sasa wamekuwa na timu nzuri sana na wamekuwa wakishinda mfululizo.
“Lazima tucheze kiakili sana, lakini naamini tutawakamata hata mwaka jana, Man City ilishinda mechi zao tano za mwanzo.”

Arsenal waliutawala mchezo wao dhidi ya Hull City na hakukuwa na shaka kabisa kuhusu kushinda mchezo huo hasa baada ya Jake Livermore kutolewa kwa kadi nyekundu kabla ya mapumziko. Lakini, Wenger anawaambia wachezaji wake kukaza buti ili kufanya vizuri kwa mechi zao za nyumbani pia.

“Tunapocheza ugenini, tunakuwa kwenye kiwango kizuri sana,” alisema Wenger.
Wenger alimsifu pia kiungo wake Alex Iwobi na kumwambia anapaswa kucheza kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa kwa mjomba wake Jay Jay Okocha alivyokuwa akitesa kwenye kikosi cha Bolton. Iwobi alikuwa staa wa mchezo huku mabao ya Arsenal yakifungwa na Alexis Sanchez (mawili), Theo Walcott na kiungo wa shoka, Granit Xhaka. Wakati mambo yakiwa matamu kwa Wenger na Arsenal yake ambayo kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, mpinzani wake Jose Mourinho na Manchester United yake ni majanga, wakiporomoka hadi kwenye nafasi ya saba baada ya vipigo viwili mfululizo kwenye ligi hiyo. Man United imeruhusu mabao matano kwenye mechi mbili za ligi za karibuni, huku yenyewe ikiwa imefunga mawili tu na kuonyesha hali ya hatari kwa miamba hiyo ya Old Trafford.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire