Google tag

dimanche 11 septembre 2016

MTOTO WA LIONEL MESSI KUANDIKISHWA BARCELONA

MTOTO wa staa wa Barcelona, Lionel Messi, Thiago Messi anajiandaa kuwa miongoni mwa watoto wa kwanza kuandikishwa katika shule ya soka ya Barcelona kwa watoto walio chini ya umri wa miaka sita kwa ajili ya kuandaliwa kuwa mastaa wa timu hiyo.
Thiago mwenye umri wa miaka minne anatabiriwa kufuata nyayo za baba yake na tayari Barcelona ina nia ya kumwandikisha katika shule yao maalumu ya FCBEscola ambapo inaruhusu watoto wenye umri wa miaka sita kuandikishwa na kujifunza mbinu za soka.
Messi (28) ambaye naye alipitia katika shule hiyo amekiri kwamba hana uhakika kama mwanaye huyu ambaye atafikisha miaka minne rasmi Novemba ana kipaji cha soka lakini anatazamia kumwingiza katika mpango huo na kuona kama atajikita katika mchezo huo ambao umempatia.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire