Leo tunaungana na mashabiki wa Hiphop duniani kote kumkumbuka rapper, Tupac Amaru Shakur ‘2PAC’ kifo chake ambacho kilitokea tarehe na mwezi kama wa leo September 13 1996, kuna baadhi ya picha ambazo hujawahi kuziona za msanii huyo.
Mwaka 1995 mwezi Marchi kulikuwa nampiga picha mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Gobi. M. Rahimi, alikuwa ndiye mpiga picha aliye mpiga 2pac mpaka siku ya kifo chake kinatokea, Mpiga picha huyo ameamua kutumia fursa hiyo ya kumkumbuka msanii huyo ikiwa ni miaka 20 tangu kifo chake kitokee.
Rahimi ni moja ya wapiga picha ambao wanafanya kazi ya kutengeneza frame za picha katika mtandao wa Sonic Editions Website na hii inaweza kuwa opportunity ya kuingiza mkwanja kupitia picha hizo.
Picha hizo zilizopigwa na Gobi, ni picha ambazo zimepigwa kwenye miaka ya 1994 wakati 2Pac anaperforme Chikago na zingine ilikuwa ni mwaka 1995.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire