Lionel Messi amefunga hat-trick wakati Barcelona ikiaangamiza Manchester City kwenye mchezo wa Champions League wakati Pep Guardiola akirejea kwenye klabu yake ya zamani.
City walipambana kipindi cha kwanza lakini walifanya makosa mengi ya wazi dhidi ya kikosi cha Barcelona ambacho ndani yake kilikuwa na Messi aliye rejea kutoka majeruhi.
Fernandinho alianguka ndani ya box na kumpa nafasi Messi kupachika bao la pili kabla ya Kelvin de Bruyne kupoteza mpira na kumruhusu Iniesta kumtengenezea muargentina huyo kufunga bao la pili.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa wageni ambapo golikipa wao Claudio Bravo alizawadiwa kadi nyekundu kwa kudaka mpira akiwa nje ya box kisha dakika moja baadaye Messi akapachika bao jingine.
Barcelona pia walibaki 10 uwanjani kwa dakika 15 za mwisho baada ya Jeremy Mathieu ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Gerrard Pique kuoneshwa kadi ya pili ya njano kwa kumfanyia madhambi Raheem Sterling.
Willy Caballero aliokoa mchomo wa Neymar lakini nyota huyo wa Brazil akafunga goli dakika moja baadaye kukamilisha ushindi wa magoli 4-0 wa miamba hiyo ya La Liga.
Ushindi huo uaifanya Barcelona kuendeleza ushindi kwa 100% katika Kundi C na kuendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi tano na Manchester City.
Hiki kilikuwa ni kipigo kingine kwa Guardiola akirejea Nou Camp. Akiwa kocha wa Barcelona, aliisaidia timu hiyo kutwaa jumla ya mataji 14 lakini sasa amepoteza mara mbili dhidi ya klabu hiyo ya Hispania. Alichezea kichapo cha magoli 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions Legue akiwa kocha wa Bayern Munich.
*Lionel Messi amefunga magoli 15 katika mechi 13 za Champions League dhidi ya timu za England.
Manchester City wamechezea kipigo kikubwa zaidi kwenye michuano ya Champions League, kwa mara ya kwanza wamefungwa magoli manne.
*Goli la kwanza la kwenye mchezo huo lilikuwa ni goli la 100 kwa safu ya MSN kwenye mashindano yote kwa mwaka 2016.
*Messi kwa sasa anaongoza orodha ya wafungaji katika viwanja vya nyumbani kwenye michuano ya Ulaya akiwa mefunga magoli 50.
Pep Guardiola ameruhusu magoli 9 kwenye mechi tatu za Champions League dhidi ya Barcelona tangu alivyoondoka kwa miamba hiyo ya Catalan.
*Barcelona wamekosa mikwaju 11 ya penati kati ya 27 ambayo wamepata katika michuano yote tangu kuanza kwa msimu wa 2015-16.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire