Superstar wa Barcelona Neymar Jr ameendeleza rekodi yake ya kupachika mabao kwenye timu yake ya taifa wakati Brazil ikiichapa Bolivia kwa bao 5-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Neymar alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 11 na ku-assist magoli mengine mawili katika kikosi cha Tite.
Goli lake dhidi ya Bolivia lilivunja rekodi ya Zico na sasa amekuwa mchezaji wa nne mwenye magoli mengi kwenye historia ya timu ya taifa ya Brazil akiwa ameshafunga magoli 49.
Wachezaji watatu wa juu yake ni Romario (55), Ronaldo (62) na Pele (77).
Lakini mchezo huo haukumalizika salama kwa upande wa Neymar baada ya kupigwa kiwiko na mchezaji wa Bolivia Yasman Duk.
Neymar alijikuta akichezea ‘kipepsi’ wakati alipojaribu kumpiga ‘tobo’ Duk lakini beki huyo wa Bolivia akampiga kiwiko cha usoni nyota wa klabu ya Barcelona lakini mwamuzi hakuamua tukio hilo liwe ‘faulo’
Damu nyingi ilitoka usoni kwa Neymar ambaye alishindwa kuendelea na mchezo na kupelekea kupumzishwa halafu nafasi yake ikachukuliwa na kiungo mshambuliaji wa Chelsea Willian.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire