#Refa wakike mrundi Suavis IRATUNGA ameorodheshwa kwenye orodha ya warefa 11 wa kati watakao simamiya michuano ya 10 ya CAN yatakayo anza rasmi tarehe 19 Novemba hadi 3 Decemba 2016 nchini Cameroun . Kwenye jumla ya warefa 11 na warefa wapembeni 14 , mwanadada Suavis atakuwa ni balozi wa Burundi kwenye michuano hiyo. Fahamu yakwamba itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki kwenye Kombe la Afrika ,ila alikuwa tayari kisha chezesha michuano kadhaa nchi mbali mbali kama Ethiopia , Guinea-Equator , Djibouti, Uganda kwenye Cecafa Women cup nakusimamiya fainali iliyo zipambanisha Tanzania na Uganda . Amejaliwa piya kuchezesha mechi nyingi kwenye ligi ya taifa nchini ,vile vile alibahatikiwa kupata mafunzo tiki tiki kwenye nchi tofauti kama Misri na kungineko.
N.B : Orodha kamili ipo hapo kwa hizo picha
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire