Google tag

vendredi 2 décembre 2016

Bob Junior ana mchango mkubwa kwenye maisha yangu – Diamond

Diamond hafanyi tena kazi na Bob Junior, lakini hawezi kusahau ukweli kuwa producer huyo wa Sharobaro Records ndiye aliyemfungulia njia ya mafanikio kimuziki.

Akizungumza kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz Alhamis hii kupitia EATV, Diamond alikiri kuwa Bob Junior ana mchango mkubwa kwenye maisha yake.

“Kiukweli Bob Junior ana mchango mkubwa sana katika katika maisha yangu kwasababu ukiangalia nyimbo zangu zote zilizonitoa ni yeye ndiye alikuwa ametengeza,” alisema Diamond.

“Japokuwa hata kipindi ambacho nilikuwa nazitengeneza inawezekana watu walikuwa hawajamuona kama anaweza kuwa producer mzuri sana. Lakini mimi nilikuwa naona mbona huyu natoka naye, nakufa naye mimi yaani huyu natoa nyimbo na inahit,” aliongeza.

“Nakumbuka tulifanya nyimbo kama sita, Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Binadamu, nyimbo tofauti tofauti. Kila nyimbo alikuwa akinitengenezea akinipa beat nikifika nyumbani naandika vibaya sana. Na mpaka nakumbuka ilifika time niliweka kama chuki fulani kwa wasanii waliopo pale wakaona mbona unampendelea mtu fulani, yeye akasema mimi ni producer, natengeneza beat nikimpa msanii kaandikie kitu kikali, akasema huyu nikimpa analeta beat kali.”

Kwa upande mwingine staa huyo alidai kuwa Mbagala ni moja ya nyimbo zake anazozipenda sana kwakuwa aliuandika kwa ufanisi mkubwa.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire