Mchezaji wa klabu ya West Ham na timu ya taifa ya Senegal, Diafra Sakho hatacheza katika mechi ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika baada ya kuripotiwa kuwa hatacheza kwa kipindi cha wiki nane zaidi kutokana na jeraha.
Klabu ya West Ham ilitoa taarifa tarehe 30 mwezi Novemba kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 hatacheza kwa wiki sita ikimaanisha kuwa hatarejea uwanjani hadi kati kati ya mwezi wa Januari.
Lakini koacha wa West Ham Slaven Bilic, amesema kuwa Sakho huenda asicheze kwa kipindi cha wiki nane na huenda sasa akarejea kati kati ya mwezi Februari.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire