Google tag

vendredi 30 décembre 2016

Dully Sykes: Baada ya miaka 3 au 5 nitawapatanisha Alikiba na Diamond

Msanii mkongwe na mtayarishaji wa muziki nchini, Dully Sykes amedai kuwa baada ya miaka mitatu au mitano kupita atakuwa na uwezo wa kulimaliza bifu la Diamond na Alikiba.


Hitmaker huyo wa ‘Inde’ alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumanne hii kuwa kuwapatanisha wasanii hao kwa sasa ni ngumu kwakuwa kila mmoja anataka sifa na kuwa juu zaidi ya mwingine.


“Kuwapatanisha inawezekana lakini si kwa sasa,” alisema. “Hii waliyofikia ni sifa kila mtu anataka sifa na kila mtu anataka kuwa mkubwa, kwahiyo mimi nitasubiri baadaye kidogo itakapofikia muda kama miaka mitano hivi mbele au mitatu Mungu akipenda na vuguvugu hili litakapokwisha mimi nina uwezo wa kuwakutanisha na kuwaambia ugomvi umekwisha. Lakini kwa ugomvi wao kupatana leo au kesho kwa sasa si kweli,” aliongeza.

Dully aliongeza kuwa kwa sasa ni ngumu kuwapatanisha wasanii hao kwa kuwa nyuma yao kuna watu wengi ambao wote kwa pamoja kuelewana kwa sasa itakuwa ni ngumu.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire