Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amekiri itakuwa vigumu mno kwa timu yake kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu kwa sababu ya tabia ya Chelsea kupaki basi.
Man United ambayo ipo katika nafasi ya sita ipo nyuma ya Chelsea kwa jumla ya pointi 13, ambao wameshinda mechi zao 11 za mwisho na kuizidi Liverpool inayoshika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi sita.
Mourinho amesema kuwa haitakuwa rahisi kwa klabu yake ya Man United kuzifikia alama ya klabu yake ya zamani, hasa ukizingatia Chelsea wanacheza mchezo wa kukaba zaidi.
“Ni vema kuwa mkweli na kusema kwamba ni ngumu sana (kutwaa ubingwa msimu huu). Si tofauti ya alama tu, bali pia falsafa ya Chelsea katika uchezaji. Hawajali nini watu wanasema, wala wanachofikiria watu. Wao wanataka kushinda tu. Na kwa sababu hiyo, sidhani kama watapoteza pointi.”
Mechi nne za mwisho kati ya sita walizoshinda Chelsea wamepata ushindi wa 1-0.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire