THAMANI YA MWANAMKE
Mwanamke, akilala na hali mumewe
amemkasirikia, basi hulaaniwa na Malaika
usikukucha.
🌼Lakini sikujuwa kua kuna na kinyume chake.
Ilitokea katika khutba ya Ijumaa, lilitokea
jambo ambalo si lakawaida, jamaa mmoja
alimshitaki mkewe kwa Shekhe wa msikiti
mbele ya watu. Shekhe akamjibu kua
mwanamke yuwabeba na yuwavumilia
mambo mengi kumshinda mwanamume
kwa mara zaidi ya mia na mia, na hata lau
angekua huyo mwanamume ana misiba au
matatizo mengi na akasubiri, lakini subira
za mwanamke ni kubwa zaidi.
Hapo hata sauti ya huyo Shekhe ilianza
kubadilika alipokuwa anamsemesha huyo
mwanamume alomshitaki mkewe na
kumwambia:
Mkeo amebeba mambo yako na ya
watoto wako, na anasimama kwa miguu
yake kuwatengezea chakula chenu. Na
Mtume (s.a.w.) ameshausia hivo.. Jee
kwani hana haki yeye ya kuheshimiwa? Na
ya kuthaminiwa? Bila ya kumpunguzia
chakula au kitu chochote anacho kihitaji?
Basi naapa Wallahi lau mwanamume
anamkasirisha mkewe, akamgeukia na
kumpa kishogo akatoka nyumba kumwacha
mkewe na huzuni, basi Mwenyezi-Mungu
anamlaani kwa kila khatwa anapokwenda,
na kumyimia rizki yake, na kumpunguzia
afiya yake, na kumuandikia kwa kila chozi
moja linalotoka machoni mwa mkewake
huyo, makaa ya moto elfu moja kila siku,
nusu yake duniyani, na nusu kesho
akheera.
Natamani maneno haya yawafikie wanaume
wengi walokwisha owa...
Machozi mangapi mengi yashamtoka
mke wako na wewe hata hujali kabisa, wala
huna hamu ya kitu chochote, wala hutaki
kujua habari yake..
Musiyawache maneno haya kubakia
moyoni mwenu tu, bali kila mtu awatumie
walokwisha owa. Na ambao hawaja owa
wahifadhi maneno haya msitari msitari
kama akiba ya kesho yake watakapo owa.
Amesema Amiir Talaal Ar-Rashiid,
Mungu amrehemu,:
(( Kama aliumbwa mwanamke kuwa ndege
angekuwa ni "Tausi", na kama aliumbwa
kuwa mnyama angekuwa ni
"Paa" (Ghazala),
na kama aliumbwa kuwa mdudu angekuwa
ni "Kipepeo" (Butterfly), lakini ameumbwa
kuwa mtu, kwa hivo yeye ndiye Mpenzi, na
ndiye Mke, na ndiye Mama bora, na ndiye
Neema nzuri kabisa ya mwanamume katika
duniya hii.
Na kama hangelikuwa mwanamke ni
kiumbe bora na kikubwa sana, Mungu
hangemfanya kuwa Huril-ayn na kutuzwa
watu Waloamini kesho Peponi.
Hakika nimependezewa na Mwanamke
kwa kuwa: "Ni kiumbe ambaye unaweza
kuishi naye kwa urahisi na vilevile kwa
vigumu kabisa, unaweza kumridhisha kwa
ua moja la waridi, na unaweza kumuuwa
kwa neno moja.
Jitahadhari ewe mwanamme ujue kuwa
mwanamke ameumbwa kwa mfupa wa
ubavu wako si kwa mguu wako hata
umkanyage...wala si kwa kichwa chako
hata umpandie juu ya kichwa chake, lakini
ameumbwa kwa mfupa wa mbavu zako ili
umueke ubavuni mwako, na ni kwa mfupa
ulioko karibu na moyo wako ili upate
kumpenda.
Mwanamke ni kiumbe bora kabisa...
Katika utoto wake humfungulia babake
mlango Peponi...
Na katika ujanajali wake humtimizia
mumewe dini yake...
Na anapokuwa mama, Pepo huwa chini
ya miguu yake...
Maneno mazuri kabisa.....
Nampa salamu na pongezi kila ambaye
ni Mwanamke.
Shukran kwa kila aloyaandika maneno
haya, na kila aloyatuma na akaingiza furaha
katika moyo wa kila msichana, na kila
ndugu wa kike, na kila mke, na kila mama.
🌷
Mola wetu tupe kutoka kwa wake zetu
watoto wenye kufurahisha macho na nyoyo
zetu...Aaamiin.
🌷🌷🌷🌷🌷🌷
Swala na Rehema za Mwenyeezi-Mungu
zimfikie Nabii wetu Mohammad, na ahli
zake na maswahaba zake wote.