Alibaba

lundi 16 mai 2016

Je nini hukmu ya mtu aliyefungulia funga ya Ramadhan kwa kuzini

*📘SWALI LA " 1137"📘*

*✍Je nini hukmu ya mtu aliyefungulia funga ya Ramadhan kwa kuzini❓ Je inampasa kutoa kafara❓*
🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷

         *📘 JAWABU 📘*

➡ Ni ubaya ulioje kwa mja muovu mwenye kukosa haya na heshima kwa Mola wake *ﷻ.*

➡ Vipi afungue saumu ya siku yake nzima hiyo kwa maasi makubwa na machafu kama hayo❓

➡Nini faida na malengo ya funga yake ikiwa amefanya jambo hilo❓

➡Ikiwa amefanya jambo hilo atapata dhambi kubwa,  na atakuwa ameharibu amali yake hiyo ya saumu ya siku hiyo.

➡ Na ikiwa amefanya zinaa hiyo baada ya kuwa muda wa saumu umemaliza kwa kuingia tayari wakati wa magharibi, hapo kuna ikhtilafu baina ya maulamaa kuhusu kuharibika saumu yake kwa maasi hayo.

➡ Na kuharibika saumu ya siku hiyo ni kauli yenye nguvu zaidi,  kwa kuwa ALLAAH ﷻ amekataza kuharibu amali zetu kwa maasi ya aina yoyote.

*➡ Amesema ALLAAHUﷻ,*

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ)
[Surat Muhammad 33]

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu.

➡ Na hata maneno ya kusimbulia pia yanaharibu malipo ya sadaka ya mja.

*Amesema ALLAAHU ﷻ*

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُمْ بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنْفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ)
[Surat Al-Baqara 264]

Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.

➡ Ikiwa kauli inaharibu sadaka,  vipi itakuwa hali katika jambo chafu zaidi kulikoni yote hayo❓❗

➡Na ALLAAH ﷻ  akakubali matendo ya waja wema tu wenye uchamungu.

➡ Amesema ALLAAHU ﷻ  baada ya kutaja kisa cha watoto wawili wa Nabii Adam A.S, ambao mmoja wao alimuua mwenzake :

(وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ)
[Surat Al-Maeda 27]

Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu.

➡ Anatakiwa kwa wajibu mtu huyo afanye yafuatayo:

1⃣Atubie kwa ALLAAHﷻ toba ya kweli.

2⃣Arudie kufunga siku hiyo kwa salama ya dini yake.

3⃣Hakuna kafara yoyote ya kutoa ikiwa amefanya zinaa hiyo baada ya kuzama jua na kuwa ni wakati wa halali kula kwa aliekuwa amefunga.

➡ Na Nakumbusha pia kuwa : " Ni haramu kisheria kwa muisilamu yoyote kufungulia saumu yake kwa kutumia kitu chochote kilicho haramishwa na ALLAAH ﷻ"

➡ Hata ikiwa atafungua kwa kuvuta sigara au kunywa pombe / ulevi,  au kumbusu mwanamke alie haramu kwake kumbusu,  au kutazama picha za Uchi,  au kutukana na mfano wa hayo.

*➡ TUNAMUOMBA ALLAAH S.W ATUFUNDISHE YALIYO NA MANUFAA NA ATUNUFAISHE KWAYO.*

📘 ALLAAHU AALAMU.

*📘JAWABU KUTOKA KWA:*
   *U / SHAABAN ALBATTAASHY.*
🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷

*👉"Ukikosa haya kwa Mola basi fanya utakayo uone atakayo kufanyia Mola"*