Alibaba

samedi 3 septembre 2016

Desiigner afunguka mziki anao fanya

Msanii Desiigner kutoka Marekani amefunguka na kusema kuwa mziki anao fanya siyo wa Rap, anaungana na Fetty wap katika swala hilo ambaye na yeye aliwahi kusema kuwa mziki anao fanya siyo wa Rap.
Desiigner mwenye miaka 19, alifunguka hayo kupitia video ya Tidal DNA series nakusema kuwa muziki wake anaoufanya sio Rap bali muziki wa msanii tu na amefunguka pia kuwa hata washikaji zake anaokaa nao hawamchukulii kama ni Rappers bali ni msanii.

Chris Brown achomolewa kwenye tamthilia ya Power kwa ukorofi wake

Chris Brown amenyang’anywa tonge mdomoni baada ya kupigwa chini kwenye tamthilia ya 50 Cent, Power, siku chache tu kabla ya kudaiwa kumtishia msichana kwa bunduki.
Vyanzo vimeiambia tovuti ya Page Six kuwa 50 alikuwa amemwahidi mshkaji wake huyo nafasi ya kuonekana kwenye tamthilia hiyo ya Starz lakini mabosi wake wameuchinjia baharini mpango huo.
Vyanzo vilivyo karibu na Brown vimesema,

“50 promised Chris a big role on ‘Power,’ playing a drug dealer. But 50 didn’t consult the network first, and execs were not happy when they found out about it.”
Kiliongeza, “The network insisted that Chris’ casting was not going to happen, because of fears about his anger issues. There was a big blowup, and they had to tell Chris he was not going to get the role. The news was delivered to him early Monday. He was livid.”

Jumanne hii Chris Brown alikamatwa na polisi baada ya msichana aitwaye Baylee Curran kudai alimtishia na bunduki. Alitoka kwa dhamana ya $250,000.
50 Cent na Brown ni marafiki na wamesharekodi ngoma kibao pamoja. Kupitia Instagram, 50 aliandika:
That’s my boy. I watched him come up, a lot of the s - - t he go threw [sic] is crazy to me . . . If someone calls 911 and says you pulled a gun on them in your house, are the police coming to creat [sic] a bunker at the end of your drive way for 11 hours to wait for a search warrant? Then live stream it, This must be VIP Treatment. SMH.”
Alhamis hii, 50 Cent aliendelea kusisitiza kuwa Brown ataonekana kwenye show hiyo “Tune into ‘Power’ next season, because you will see Chris Brown,” aliiambia Page Six.