Alibaba

samedi 29 octobre 2016

Cristiano Ronaldo: Ashley Cole ndio beki mgumu sana kumpita

Mchezaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Ureno anaye chezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo baada ya kufanya mahojiano na jarida la Coach Magazine na kufunguka mambo kadhaa kuhusu soka, katika interview hiyo Ronaldo kazungumza alichojifunza katika soka na kamuongelea mpinzani wake Lionel Messi pamoja na beki Ashley Cole.

*Qn.* Kitu gani kikubwa ambacho mchezo wa mpira wa miguu umekufunza?

*Ans.* Kutumia mawazo hasi ya watu wanaokupiga kukuhamasisha, kiukweli nawahitaji haters kwa sababu wamenisaidia kufanikisha kila kitu nilichofanikiwa.

*Qn.* Kuhusu Lionel Messi?

*Ans.* Kuna heshima kubwa sana kati yangu na Lionel Messi, lakini vyombo vya habari vinapenda tuonekane kama tunaupinzani mkubwa sana lakini hatuna upinzani huo, haina maana kama sisi ni marafiki wa karibu sana lakini kuna heshima kubwa kati yetu

*Qn.* Ni beki gani mgumu ambaye amekuwa akikupa wakati mgumu

*Ans.* Ashley Cole ndio beki mgumu sana kumpita niliyewahi kukutana nae.
Cole na CR7 wameshakutana kuanzia kwenye ngazi ya taifa mpaka kwenye vilabu, wakati CR7 akiwa Old Trafford na Cole akiwa Gunners na baadae The Blues.