Alibaba

mercredi 16 novembre 2016

Adhabu ya kifo dhidi ya Mohammed Morsi yatenguliwa

Mahakama ya juu nchini Misri imetengua adhabu ya hukumu ya kifo dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi.
Morsi alihukumiwa adhabu ya kifo kwa ushiriki wake wa kuvunja gereza na wafungwa kutoroka kulikofanywa mwaka 2011 wakati wa vuguvugu la mabadiliko lililoikumba nchi hiyo.

Alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo mwaka 2012, lakini aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wake kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika nchini humo kuupinga utawala wake.

Kwa nyakati tofauti Morsi alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ugaidi na bado anakabiliwa na mashitaka mengine.

For more click :

Share on whatsapp

Lampard: Kuiaga klabu ya New York City

Kiungo wa kati wa zamani wa England na Chelsea, Frank Lampard amesema ataiaga ligi ya MLS ya New York City.

Lampard mwenye umri wa miaka ,38, ambaye mkataba wake utakamilika mwishoni mwa mwaka huu , amechapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba wakati wake katika klabu hiyo ''umefika kikomo.''

Amesema atatangaza hadharani ' hatma yake ya siku zijazo' hivi karibuni.''

Lampard amefunga mabao 15 katika mechi 31 alizoshiriki katika klabu ya New York ,kwa miaka miwili iliyokatizwa na mkopo kutoka Manchester City.

New York City walifungwa mabao 7 kwa nunge na klabu ya Toronto FC katika hatua za kwanza za mwezi.
Lampard alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2014, na kuvunja rekodi ya mabao 211.

Mwenzake wa timu ya timu ya Uingereza na Liverpool Steven Gerrard pia anaweza kumaliza muda wake nchini Marekani
Gerrard, 36, amesema amekamilisha mkataba wake kwa akiichezea klabu ya LA Galaxy na amesema anaweza kuhudumu kama mkufunzi kwa klabu yake ya Liverpool.

Usain Bolt kujiunga na Borussia Dortmund

Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund imesema kuwa mwanariadha wa mbio fupi kutoka Jamaica Usain Bolt atashiriki mazoezi na klabu hiyo kwa siku chache.

Bolt amekuwa akisema kwamba angependa kucheza soka baada ya kustaafu katika riadha.

Lakini wakimkaribisha, maafisa wa klabu hiyo wamesema kuwa hakuna hakiksho kwamba mwanariadha huyo ataichezea klabu hiyo katika siku za usoni.

Messi na wenzake wagomea

Lionel Messi amewaongoza wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina kususia kuongea na wanahabari baada ya uokosoaji kuhusu uchezaji duni wa timu hiyo.
Messi, 29, alitangaza mgomo huo baada yake kufunga bao wakati wa ushindi wao wa 3-0 mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Colombia.

Kituo kimoja cha redio kilikuwa kimeripoti kuwa mshambuliaji Ezequiel Lavezzi alivuta bangi baada ya kipindi cha mazoezi, tuhuma ambazo amekanusha.
"Tumepokwa tuhuma nyingi, kukosewa heshina na hatujasema lolote," messi alisema.

Messi na wenzake 25 waliondoka kutoka kwenye kikao na wanahabari bila kuzungumza nao baada ya mechi hiyo dhidi ya Colombia.

Taarifa zinasema Lavezzi atakishtaki kituo hicho cha redio.
"Tunajua wengi wenu ambao hamna heshima kwa mchezo huu, lakini kuingilia maisha ya kibinafsi ya mtu mmezidi," Messi aliongeza.
Argentina walikosolea sana baada yao kulazwa 3-0 na Brazil lakini ushindi wao dhidi ya Colombia umewawezesha kupaa hadi nambari tano na kwenye nafasi za kushindania kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Mataifa manne yanaomaliza juu kanda ya Amerika Kusini hufuzu moja kwa moja. Nambari tano hukutana na mpinzani kutoka bara jingine kuamua mshindi.

Donald Trump kulipwa $1 kila mwaka

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000 atakapochukua hatamu Januari mwakani. Badala yake atakuwa akilipwa $1 pekee kila mwaka.
Alifichua mpango wake huo wakati wa mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes cha CBS News.

Ingawa hakujua rais huwa analipwa pesa ngapi, Bw Trump alisema alidhani anahitaji kuchukua tu $1.
Baada ya Bi Stahl kumjulisha kwamba mshahara wa rais ni $400,000, alisema: "Hapana, sitaupokea mshahara huo. Sizichukui kamwe."

Rais huyo mteule anatimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni.
Aliambia waliohudhura mkutano wake Septemba kwamba mshahara wa rais si jambo kubwa kwake.

Kuna viongozi wengine walioukataa mshahara?

Bw Trump si kiongozi wa kwanza wa Marekani kukataa mshahara.

Herbert Hoover, aliyekuwa ametajirika kupitia biashara ya madini kabla ya kuingia madarakani, na John F Kennedy, aliyerithi utajiri mwili, wote walikataa kupokea mashahara na badala yake wakatoa pesa hizo zisaidie wasiojiweza katika jamii.
Meya wa zamani Michael Bloomberg, gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger na gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney pia walikataa kupokea mishahara yao.
Mark Zuckerberg, mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, ndiye mfanyakazi anayelipwa mshahara wa chini zaidi katika kampuni hiyo.

Aidha, ni miongoni wa CEO (Afisa Mkuu Mtendaji) wengi ambao hulipwa mshahara wa $1 pekee.
Sergey Brin na Larry Page wa Google pia wamekuwa wakilipwa $1 kwa mwongo mmoja sasa.

Larry Ellison wa Oracle pia aliukataa mshahara wake kwa miaka kadha alipokuwa CEO. Afisa mkuu mtendaji wa Hewlett Packard Enterprise (HP) Meg Whitman apia alichukua hatua sawa.

Viongozi hawa hata hivyo hujipatia pesa kupitia njia nyingine. Wengi ni kupitia hisa wanazomiliki na wengine hulipwa kwa kutegemea matokeo au mapato ya kampuni.

Viongozi wa nchi nyingine hulipwa pesa ngapi?

Licha ya $400,000, anazolipwa rais wa Marekani, pia hupewa jumla ya $50,000 ambazo huwa hazitozwi ushuru, kwa mujibu wa sheria.
Waziri mkuu wa Canada alilipwa C$340,800 (£201,202) mwaka uliopita.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alilipwa $242,000 (£193,976) naye Rais wa Ufaransa Francois Hollande akalipwa $198,700 (£158,000), kwa mujbiu wa taarifa ya CNN ya mwezi Agosti.

Bw Hollande alipunguza mashahara wake kwa 30% alipoingia madarakani mwaka 2012.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May hulipwa $186,119 (£143,462) kila mwaka, ingawa thamani yake kwa dola imeshuka baada ya Uingereza kupiga kura kujiondoa EU.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza David Cameron alishutumiwa sana alipoongeza mshahara wake kwa 10% mwaka 2015.

Hata hivyo alisema jambo la busara ni kulipwa "mshahara unaolingana na kazi".
Aliongeza kwamba kuongezewa mashahara kulimpa uwezo zaidi wa kutoa pesa za hisani na mambo mengine ya kusaidia jamii.

Wazo hili lilitoka wapi?

Mwanzilishi wa Apple Steve Jobs alivumisha wazo la mshahara wa $1 Silicon Valley baada yake kurejea katika kampuni hiyo 1997.

Wakuu wa kampuni mbalimbali wamekuwa wakikosa kupokea mishahara yao tangu Vita Vikuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia.
Wakuu wa kampuni, benki na viwanda mbali ambao walijitolea kutumikia nchi katika majukumu mbalimbali wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia walifahamika kama "wanaume wa dola moja kila mwaka". Kwa kuwa sheria nchini Marekani huharamisha mtu kufanya kazi bila kulipwa, viongozi hao walipokea mshahara wa $1 kutimiza matakwa ya sheria kwamba walikuwa wanalipwa.

Wazo hilo lilirejea wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ambapo wakuu wa kampuni kubwa kama vile Lockheed, Chrysler na Boeing walijitokeza kutumikia nchi kama uzalendo.

Donald Trump atapata pesa wapi?

Ana biashara nyingi ambazo zinampa pesa, ingawa kwa baadhi watu wameuliza maswali. Alitangaza majuzi kwamba wanawe - Donald Jr, Eric, na Ivanka - na mume wa Ivanka, Jared Kushner, watakuwa kwenye kamati inayosimamia mpito.

Bw Trump hatakiwi kuuza mali yake, ambayo thamani yake inafikia mabilioni, lakini amesema biashara zake zitasimamiwa na watoto wake.
Lakini kuhusika kwa watoto wake katika shughuli ya mpito kumewafanya baadhi kusema kutakuwa na mgongano wa maslahi.
Isitoshe, Bw Trump bado hajatoa taarifa zake za kodi na hakuna ajuaye iwapo kuna wato kutoka nje wanaomiliki sehemu ya hisa aktika biashara zake. Hilo linaweza kuathiri uhusiano wa Marekani na nchi za nje, hivyo kuibua suala la mgongano wa maslahi.

Jokate, Brown Mauzo, Abdu Kiba na wengine kuanza kuachia kazi chini ya label ya Alikiba ‘King’s Music’

Alikiba ametaja wasanii ambao wapo chini ya lebel yake ya ‘King’s Music”

Alikiba amewataja Jokate, Abdu Kiba, Delila, Abby Skills na Brown Mauzo wa Kenya kuwa ni baadhi ya wasanii ambao wapo chini ya label yake ambayo ameedai ipo tangu siku yingi lakini hakuitangaza tu.

“Mimi Record label ninayo muda mrefu,muda mrefu sana lakini sikufanya matangazo lakini nina wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi nimerudi tena najipanga upya nao waendelee kufanya kazi, kama ambavyo unamuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea kufanya kazi, pia kuna Abdu Kiba” Alikiba alifunguka kwenye 255 ya Clouds Fm.

“Afu vilevile kuna msanii mwingine ambao watu hawajawahi kumsikia, Pia kuna wakiana Jokate, kina dalila na wengine wengi wapo chini ya label yangu, sijafanya rasmi lakini mtawasikia.”