Raisi mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka
kabisa.Infantino anaonekana kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta
vyake.Baada ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026
kufikia timu 48 sasa Infantino amekuja na mpya.Kwa kumtumia mkurugenzi
wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten amependekeza baadhi ya
sheria mpya katika soka.
Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.
“sipati picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi
nyingi sana za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa
wakuvutia sana kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo
litawafurahisha mashabiko na washambuliaji.
Kubadili upigaji wa penati.Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa
FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati.Kwa sasa adhabu ya penati
mchezaji anauweka mpira mita kadhaa karibu na goli ma kuupiga.Lakini Van
Basten anaona penati ibadilishwe.Anataka mpiga penati auweke mpira mita
25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda
usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio ngeni kwani mwaka
1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.
Kupunguza adhabu mipira ya kushika.Van Basten anaona kama adhabu ya
kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo.Na analiona kama tukio dogo
lisilohitaji kadi nyekundu na anazani inapaswa ipunguzwe adhabu
hiyo.Kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa.Adhabu kam ile ya tukio la
Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika mpira wakati
ukiingia golini Van Basten anataka kadi iwe ya njano.
Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi.Kama katika Rugby ni kapteni
tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji yeyote kuongea
na mwamuzi.
Style ya faulu ya mchezo wa kikapu.Katika mchezo wa kikapu pale mchezaji
anapocheza faulu tano anatakiwa atoke uwanjani.Na sasa Van Basten
anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.
Kupunguza idadi ya mechi.Hii itafurahiwa sana na makocha wageni
Uingereza.Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi ya
mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe
kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.
Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani kuongeza idadi ya
wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa
wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba na sasa FIFA
inatarajia kuliangalia suala hili.
Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua kutokana na
kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya upigaji penati
vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha dakika 10 za
mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema watahakikisha hakuna
upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.
Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA, na
sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze
kujadiliwa.