Mwamuzi Mark Clattenburg ameteuliwa kuchezesha mechi ya Chelsea dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield wiki ijayo.
Chelsea watasafiri hadi Anfield wiki ijayo siku ya Jumanne (Januari 31) wakiwa na pointi 10 dhidi ya timu ya Jurgen Klopp.
Clattenburg ana historia kadhaa anapo chezesha mechi za Chelsea, mechi ya mwisho msimu uliopita katika uwanja wa Stamford Bridge dhidi ya Tottenham Hotspur ikizua utata.
Kadi kumi na mbili za njano zilitolewa katika pambano hilo, na vitendo vya vurugu baina ya wachezaji katika sare ya 2-2.
Chelsea na Tottenham zilitozwa faini ya paundi 375,000 na 225,000 mwenyeji kuhusika katika kile kilichotokea, lakini Clattenburg hakuweza kutoa kadi nyekundu katika mechi hiyo.
Hii itakuwa mara ya pili kwa mwamuzi huyo kutoka County Durham kuchezesha mechi ya Chelsea msimu huu, baada ya kuchezesha Blues wakishinda 3-0 dhidi ya Burnley mwezi Agosti.