Google tag

mardi 9 mai 2017

Jaji wa mahakama kuu afungwa jela India

Mahakama ya juu zaidi nchini ndia imemhukumu jaji wa mahakama kuu ya Calcutta, kifungo cha miezi sita gerezani.
Jaji Chinnaswamy Swaminathan Karnan ndiye jaji wa kwanza wa mahakama kuu kufungwa gerezani katika historia ya nchi hiyo.
Jaji Karnan, amepatikana na kosa la kudharau mahakama siku moja baada ya hatua yake ya kujaribu kumhukumu jaji mkuu wa India na majaji wengine sita wa mahakama ya juu zaidi kifungo cha miaka mitano Jela.
Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwepo na hali ya mvutano na majibizano katika mahakama ya juu nchini India.
Mwezi Januari Jaji Chinnaswamy Karnan aliwashutumu majaji kadhaa wa mahakama ya juu nchini India kwa kuwa wafisadi.
Katika shutma hizo jaji huyo wa mahakama ya juu alimwandikia waziri Mkuu waraka maalum akitaka kuungwa mkono kwa juhudi zake zake za kutaka majaji hao wa mahakama wakamatwe, wachunguzwe na kutupwa jela miaka tano kwa madai ya ufisadi.

Hata hivyo jaji huyo hakutoa ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba hao wakubwa zake ni wafisadi.
Kwanzia wakati huo uhasama kati yake na majaji wa mahakama ya juu nchini India ukazidi.
Majaji hao wakamtumia ilani wakimtaka afike mbele yao kwa kujibu mashataka ya kuwaharibia majina.
Hata hivyo alipuuza agizo hilo.
Jaji mkuu wa nchi hiyo katika siku za hivi karibuni ametoa agizo kwamba jaji huyo apelekwe hospitali kupimwa akili kwani alisema wanadhani kwamba si mzima wa akili.

Mwanafunzi anayefanana na Lionel Messi nchini Iran azua gumzo

Mwanafunzi mmoja nchini Iran amelazimika kupelekwa katika kituo cha polisi mwishoni mwa wiki iliyopita kisa na mkasa! Kufanana kulikokithiri na Lionel Messi.
Watu wengi katika mji wa Hamaden wamekuwa wakiomba kupiga picha na kijana huyo aitwaye Reza Parastesh, na hivyo kusababisha msongamano wa watu kila atakakokanyaga, hivyo polisi walilazimika kumhifadhi kwa muda ili kuondoa msongamano huo.

Mchanganyiko huo ulianza miezi michache iliyopita wakati baba wa kijana huyo aliyefanana mno na Messi alipompiga picha akiwa amevalia fulana ya timu ya Barcelona yenye namba kumi.
Reza Parastesh, ana umri wa miaka ishirini na mitano kwa sasa, hivi karibuni alianzisha mtindo wa ukataji nywele na kupunguza ndevu zake mithili ya mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina .
Reza Parastesh, kwa sasa amebatizwa jina 'Messi wa Iran' amejikuta kila wakati na kila mahali akiombwa kupiga picha na watu wa aina kwa aina katika mji wa nyumbani kwao Hameden, nchini Iran.
Kijana huyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kwa sasa watu  wananiona mimi kuwa ndiye Messi wa Iran na kunitaka nifanye kiila kitu afanyacho Messi halisi, na pindi ninapotokeza mahali, watu hupatwa na mshtuko.

Nina furaha kubwa kuona kwamba ninawapa furaha na hili linapotokea linanipa ari mpya.
Parastesh aka Messi amekuwa ni mtu mwenye kufanyiwa mahojiano ya mara kwa mara na vituo vya habari na kufanikiwa kusaini mikataba mikubwa ya uoneshaji mavazi, na sasa ana fanya mazoezi makubwa ya kujua mbinu za mpira wa miguu ili akidhi vigezo vya Messi halisi.