Jumamosi Disemba 21 mwaka huu katika mechi ya Serie A kati ya Inter dhidi ya Genoa Romelu Lukaku alimpa penati Sebastiano Esposito apige. Hilo likawa ni bao la kwanza kwa kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 katika Serie A
Kilichotokea dogo akalia kwa uchungu sana na kwenda kushangilia kwa mama yake mzazi kutokana na furaha iliyopitiliza . . .
Katika mechi hiyo waliyoibuka na ushindi wa mabao 4-0 Lukaku alifunga mabao 2 maana yake alijinyima Hat Trick akampa heshima bwana mdogo
.
.
Hilo likawa tukio kubwa la kihistoria kwa kinda huyo ambaye baada ya hapo alienda kujumuika na familia yake kusherekea kufunga mwaka kwa heshima ya kipekee. . .