Google tag

dimanche 6 mars 2022

Vladmir Putin: Africa haitokuwa huru kamwe

"Afrika haitokaa iwe HURU. Waafrika wanawaamini Wazungu, Wamarekani na Wachina zaidi kuliko wanavyojiamini wao wenyewe....hawajiamini wao wenyewe hata kidogo.


Mtu mweupe anafanya makosa Afrika tena makosa ya jinai ila hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu mamlaka za Afrika zinatutazama sisi weupe kama miungu, jambo ambalo liko mbali sana na ukweli.

Mtu mweusi (Mwafrika) anaweza kuteswa, kunyanyaswa na hata kuuawa kinyama Ulaya lakini hakuna mamlaka yoyote ya Afrika inayoweza kuuliza wala kuhoji.

Waafrika wamejikubali na kuamini kuwa wao ni watu DHAIFU wasio na tumaini haswa linapokuja suala la kupambana na Wazungu, Wamarekani na Wachina. Mzungu, Mmarekani au Mchina anaweza kumdhalilisha, kumtukana, kumpiga na hata kumuua Mwafrika katika ardhi ya Afrika tena kwenye nchi yake au nje ya Afrika na Viongozi wa Afrika wataliona hilo na kila mmoja atajiweka kana kwamba hakuona wala kusikia.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.

Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."

Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
Je ni kipi unaweza kuongeza kuhusu Afrika?
(Via Remmy Cameroon)