Msuluhishi wa Ukraine kwenye mzozo wa kivita dhidi ya Urusi, ameuawa baada ya maafisa usalama wa Ukraine kugundua kuwa alikuwa ni jasusi aliyetumika kupeleleza pande zote mbili.
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Denis Kireev amesema oparesheni hiyo ya kumuua mpelelezi huyo imetekelezwa na kitengo cha Usalama wa Taifa cha Ukraine baada ya kukataa kujisalimisha.
Urusi na Ukraine wametoa shutuma kuwa alikuwa mpelelezi aliyetumika kwa mataifa yote mawili.
Gazeti la Urusi, Pravda limeripoti kuwa Usalama wa Taifa wa Ukraine ulipata ushahidi wa mawasiliano ya jamaa huyo ambayo yaliashiria kuwa anatumika na pande zote mbili.
Kachero huyo alikuwa sehemu ya timu inayoshugulika kupatikana kwa suluhu kati ya Ukraine na Urusi.