Shinzo Abe aliingia madarakani nchini Japan 🇯🇵 mwaka 2006, akastaafu 2020, leo alikuwa akihutubia wananchi kwenye kampeni za uchaguzi.... Ghafla akatokea mwanaume huyu akampiga risasi mbili mgongoni na kufanya aanguke chini.
Kwa mujibu wa polisi, inatajwa silaha iliyotumika ilitengenezwa nyumbani.
Japan kuna sheria kali sana kuhusu umiliki wa silaha, ni moja ya nchi tajiri Duniani ambazo zinamatukio machache zaidi ya mauaji ya kutumia Silaha.
Shinzo Abe anakumbukwa kwa kufanya Mapinduzi ya kiuchumi nchini Japan.
Taarifa za awali zinadai mwanaume huyo alikuwa mwanajeshi mstaafu. Alikamatwa mara tu baada ya kutekeleza shambulio hilo kama unavyoona hapo kwenye picha.