Moja kati ya habari kubwa Wiki hii ni hii ya Bunge la Ulaya kupitisha sheria mpya ambazo zitaanzishwa katika nchi za Umoja wa Ulaya, ambazo zinawalazimu Watumiaji na Watengenezaji wa vifaa vyote kama vile smart phones, vishkwambi, camera nk kutumia charger aina ya type c ifikapo mwaka 2024, hili likiwa ni jambo la kwanza duniani ambalo linatarajia kumuathiri Mtengenezaji wa simu za iPhone na Apple zaidi ya Wapinzani wake.
Kura hiyo inathibitisha makubaliano ya awali kati ya Taasisi za Umoja wa Ulaya kuifanya USB aina ya C inayotumiwa na vifaa vinavyotumia Android kuwa kiwango pekee cha Umoja wa Ulaya na hivyo kuilazimu Kampuni kutokea nchini Marekani Apple (AAPL.O) kubadilisha sehemu zake za kuchajia simu za iPhone na vifaa vingine.
Wachambuzi pia wanatarajia matokeo chanya kwa sababu inaweza kuwahimiza Watu kununua vifaa vilivyotolewa hivi karibuni vya kampuni hiyo, badala ya vile visivyo na USB-C.
Makubaliano haya pia yataathiri vifaa vya kusomea, na teknolojia nyinginezo, kumaanisha kuwa huenda pia mabadiliko hayo yakaathiri kampuni ya Samsung pamoja na Huawei.