Alibaba

mardi 1 novembre 2022

Davido afisha mtoto wake

Mtoto wa mwanamuziki Davido Adeleke na mpenzi wake Chioma Rowland, Ifeanyi Adeleke (3) amefariki dunia baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea ‘Swimming Pool’ nyumbani kwao.


Vyombo mbalimbali vya habari nchini Nigeria vinaripoti kuwa mtoto huyo alifariki jana Jumatatu Oktoba 31, 2022.


Taarifa zinasema Ifeanyi alizama kwenye maji kwa muda mrefu kabla ya wazazi wake hawajagundua kutoweka kwa mtoto wao na baadaye walikuta akielea kwenye maji.

Davido anakuwa msanii wapili nchini humo kumpoteza mtoto kwa kuzama kwenye maji, kwani mwaka 2018 moto wa msanii D’Banj naye alipoteza maisha katika tukio kama hilo.