Kwa mujibu wa jarida la Forbes limetoa orodha ya Familia za Kifalme tajiri zaidi duniani, Licha ya kuwepo na matajiri wakubwa zaidi duniani na matajiri hao wengi wao wakitoka nchini Marekani, wakiongozwa na Mfaransa ambaye pia ni mmiliki wa kampuni kadhaa kubwa duniani kama Louis Vuitton, Moet, Dior, kampuni ya vinywaji ya Hennesy na zingine Bernard Arnault mwenye utajiri wa USD bilioni 211. akifuatiwa na Wamarekani kama 6 ambao ni Elon Musk dola bilioni 180, Jeff Benzoz dola 114 bilioni, Larry Ellison dola 107bilioni, Warren Buffet dola 106 bilioni huku Bill Gate akiwa na utajiri wa dola 104 bilioni akishika nafasi ya 7 kwa utajiri duniani.
Hali ni tofauti kwa familia za Kifalme ambapo katika famili 5 za Kifalme tajiri zaidi duniani 4 zinatoka katika mataifa ya Uarabuni.
5. Familia ya Kifalme ya Uingereza yenye utajiri wa dola bilioni 88
4. Familia ya Kifalme ya Abu Dhabi yenye utajiri wa dola bilioni 150
3. Familia ya kifalme ya Qatar yenye utajiri wa dola bilioni 335.
2. Familia ya kifalme ya Kuwait yenye utajiri wa dola bilioni 360
1. Familia ya Kifalme ya Saudi Arabia yenye utajiri wa dola Trilioni 1.4
Uhalisia ni kwamba licha ya kuwa ni familia za Kifalme ila ndio ambazo zinaongoza kwa utajiri duniani hasa famili ya Kifalme ya Saudi Arabia ikiwa na utajiri wa dola Trilioni 1.4, utajiri ambao huwezi kufikiwa na tajiri yoyote duniani.