Baruwa ya 2Pac kwenda kwa Madona

Barua ya kipekee iliyoandikwa kwa mkono na msanii mashuhuri wa hip hop, Tupac Shakur
wakati akitumikia kifungo chake katika gereza la Rikers Island mwaka 1995,

Baruwa hii imeweka wazi sababu ya 2Pac kuachana na mwanamuziki Madonna.
Katika barua hiyo Tupac alieleza kuwa uhusiano wake na Madonna ulikuwa changamoto kubwa kwa taswira yake kama kijana mweusi na msemaji wa jamii yake.
Tupac aliandika kuwa kuwa kwenye mahusiano na mwanamke mzungu, hasa maarufu kama Madonna, kungeweza kuathiri sura yake kwa mashabiki wake weusi. 
Alieleza kuwa, “Athari za ubaguzi wa rangi hufanya iwe vigumu kwa kijana mweusi kuonesha mapenzi kwa mwanamke mzungu mwenye umri mkubwa.” Akiwa na maumivu lakini pia heshima, 
Tupac alimuomba radhi Madonna kwa namna walivyoachana, akimtaja kuwa alikuwa mwenye wema na msaada mkubwa kwake.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa nafasi yake kama msanii, kiongozi wa vijana na sauti ya jamii ya watu weusi, vilifanya uhusiano huo kuwa mgumu kuendelezwa hadharani. 
Barua hiyo haikujulikana kwa umma hadi miaka kadhaa baadaye ilipowekwa kwenye mnada, na kutoa mwanga kuhusu mapambano ya ndani ya Tupac kati ya upendo wa kibinafsi na matarajio ya jamii. 

Post a Comment

Plus récente Plus ancienne