MASHABIKI wa Manchester United ya England wa mkoani morogoro wamesema ni pigo kubwa kwa timu yao baada ya Kocha Sir Alex Ferguson kutangaza kung’atuka kuifundisha timu hiyo baada ya msimu huu.
Wakizungumza na Championi Ijumaa mjini hapa, baadhi ya mashabiki hao walisema Ferguson alikuwa mtu muhimu na nguzo imara ndani ya Man U, hivyo kuondoka kwake kutaacha pengo kubwa katika klabu hiyo.
Walisema kocha huyo alikuwa mstari wa mbele kuitafutia mafanikio timu hiyo ikiwa ni pamoja na kudumisha nidhamu katika kikosi cha United.
“Kwa kweli tumepata pigo kubwa sana lakini hatuna jinsi, tunapaswa kuheshimu maamuzi yake,” alisema Mangi Chang’waro.
Hata hivyo, mashabiki hao walisema wanaomba apatikane kocha mwingine mzuri atakayeendelea kuipa mafanikio timu hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire