HIVI karibuni mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa akifuturu na
hawara yake, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kitendo ambacho kimewashangaza
wengi na baadhi kufikia hatua ya kumponda kuwa anakwenda kinyume na
Uislam.
Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza-
Mori jijini Dar ambapo mbali na mastaa hao, pia walikuwepo waumini
wengine wa dini hiyo walioalikwa katika chakula hicho kitakatifu.
Waumini wamponda
Wakizungumza na gazeti hili mara baada ya kumuona Penny ambaye ni demu
wa Diamond akiwa eneo hilo, baadhi ya waumini walisema walishangazwa na
uwepo wake kwani sheria ya dini ya Kiislam hairuhusu kuwa karibu na
kimada hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Walisema, Diamond hatakiwi kuwa karibu na Penny si kwa kipindi hiki tu
bali hata baada, mpaka pale ambapo atatoa mahari na kuozeshwa kwa
kufuata misingi ya dini ya Kiislam.
“Huyu kijana kafanya jambo zuri
la kuwafuturisha wenzake ila amekosea kumualika yule mwanamke wake, yule
kwake ni kimada na kwa sheria za dini yetu huruhusiwi kabisa
kumkaribia, sasa ona wanafuturu pamoja na wanashikanashikana, ile siyo
sawa,” alisema muumini mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Swaleh alisema: “Diamond
anatakiwa aambiwe kuwa anafanya makosa sana kuwa karibu na yule Penny.
“Kihalali kwanza anatakiwa amsilimishe kisha amlipie mahari ndipo amuoe
lakini kinyume na hapo atakuwa anaishi na hawara na kuwa naye karibu ni
kujichumia dhambi anazoweza kuziepuka.”
Mashehe nao wacharuka
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya mashehe
wenye heshima kubwa Tanzania nao walionesha kukerwa na kitendo
alichokifanya Diamond na kusema kinakiuka maadili ya dini yao.
Walisema, mwanamke ambaye hajaolewa anayeishi au kuwa karibu na mwanaume
na wakati mwingine kuzini, huyo ni kimada na hana nafasi kwenye Uislam.
Shehe Khamisi Mataka
Huyu ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mashehe na Wanazuoni Tanzania
anasema: “Lengo la swaumu ni kumfanya mtu kuwa Mchamungu na Mchamungu ni
yule anayefanya yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha
aliyokatazwa.
“Katika Uislam kuwa na hawara inakatazwa, si kwa
kipindi hiki tu cha Mwezi Mtukufu bali hata baada. Kwa hiyo kufuturu na
hawara ni kinyume na Uislam na unapata dhambi.”
Maalim Hassan Yahya
Ni Mnajimu maarufu nchini. Yeye anasema kuwa, hawara hakubaliki kidini
hivyo hatakiwi kupika futari wala kuwa naye karibu kwa namna yoyote,
kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za funga na maadili ya
Uislam.
Shekh Alhad Musa Salum
Huyu ni Shehe Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam. Kuhusiana na hili la Diamond la kufuturu na Penny
anasema kuwa, uhawara hauruhusiwi katika Uislam na wanaoendekeza hilo
waache mara moja ili waweze kupata radhi za Mwenyezi Mungu.
Shehe
Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Simba hivi karibuni aliwasihi Waislam
kutimiza nguzo hiyo muhimu ya Uislam na kuwataka wahakikishe wanafuata
sheria na taratibu zilizowekwa ili waweze kufikia lengo la kufunga
Source:GLP
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire