Google tag

lundi 23 décembre 2013

DAYNA: SITAKI MALUMBANO NA DIAMOND

Na Gladness Mallya
MWANADADA anayetamba na kibao cha Mimi na Wewe, Mwanaisha Said Nyange ‘Dayna’ amefunguka kuwa hataki kabisa kumzungumzia msanii mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mwanaisha Said Nyange ‘Dayna’.
Dayna aliyasema hayo hivi karibuni alipoulizwa kuhusiana na bifu lake na Diamond lililotokana na kumwibia wimbo wake ambapo alisema hataki kumzungumzia kabisa Diamond kwa sababu hataki malumbano kwani hivi karibuni amezungumza maneno mbofumbofu kwenye vyombo vya habari.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Mimi sitaki malumbano na Diamond  kwa sababu amekuwa akizungumza mengi sana kwenye vyombo vya habari mengine ya kuniponda na mengine ya kawaida hivyo sitaki malumbano kabisa mimi niko kikazi zaidi yeye aendelee tu”, alisema Dayna.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire