Alibaba

mardi 1 juillet 2014

hukumu ya kufunga siku ya ijumaa mosimosi pekee hatahata na inapo angukia ashuraaashuraa au arafaa


Swali LA KWANZA:

Assalamu Alaykum Warahmatullahi
Wabarakatu.
Shukran kwa kazi zenu munazofanya
kuelimisha umma.
Tumeelezewa kwamba haifai mtu kufunga
saum ya sita katika siku ya jumamosi, je hii
ni sawa. Je ikiwa nafunga saum ya 13, 14 &
15 ikiangukia jumamosi nifunge au vipi?
Shukran


SWALI LA PILI:
Eti kufungua Jumamosi haifai hata ikiwa ni
siku ya Arafa au Ashoora?


JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allaah
(Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola
Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na
salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume
Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake
(Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu
wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ahsante kwa ndugu zetu waliouliza
maswali hayo ambayo kwa nyakati za
karibuni limeleta utata sana baina ya
Masheikh na pia Waislamu wa kawaida.
Utata huu umesababishwa na kufahamika
Hadiyth hii kuwa ni ya makatazo katu, nayo
inasema:

Kutoka kwa 'Abdullaah bin Busr kutoka
kwa kaka yake kwamba Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
kasema: ((Msifunge siku ya Jumamosi
isipokuwa ikiwa mmefaridhiwa na Allah
kwenu. Ikiwa mtu hakupata chochote cha
kula isipokuwa ganda la zabibu au gome la
mti, basi alitafune)) [at-Tirmidhy, Abu
Dawud, an-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad na
al-Haakim). Al-Haakim anasema kuwa hii ni
Hadiyth Sahihi kulingana na sharti za
Muslim na at-Tirmidhy akasema ni Hasan]
Wanaokataa kufunga kwa siku hiyo
wanategemea Hadiyth hiyo.

Wale wanaosema kuwa inawezekana
kufunga siku hiyo wanategemea Hadiyth
zifuatazo. Miongoni mwazo ni: Abu Dharr
(Radhiya Allahu 'anhu) amesema: "Mtume
wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi
wa sallam) alituamuru kufunga siku tatu
katika kila mwezi – yaani masiku meupe,
ambapo mwezi unakuwa umekamilika
(tarehe 13, 14, na 15 katika miezi ya
Kiislamu).

Na akasema kufanya hivyo ni
sawa na kufunga milele” (An-Nasaaiy na
Ibn Hibbaan, ambaye amesema ni Sahihi).
Wanachuoni wanasema kuwa hii ni kauli ya
kijumla katika kufunga siku hiyo na huenda
Jumamosi ikaangukia moja ya terehe hizo.
Na pia ipo Hadiyth ambayo inatupigia
mfano wa funga ya Mtume (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) katika suala
hilo. Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya
Allahu 'anhaa) amesema: “Mtume wa
Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) alikuwa anafunga siku ya
Jumamosi, Jumapili na Jumatatu katika
mwezi mmoja na Jumanne, Jumatano na
Alkhamiys katika mwezi mwengine” (At-
Tirmidhiy).

Amesema ‘Abdullaah bin ‘Amr bin al-‘Aas
(Radhiya Allahu 'anhu) kuwa Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
alimwambia: “Funga inayopendeza zaidi
kwa Allah ni funga ya Nabii Dawud …
alikuwa anafunga siku moja na anakula
siku moja” (Al-Bukhariy, Muslim na an-
Nasaaiy).

Hii ni Hadiyth ndefu ambayo inapatikana
katika Riyaadhus Swaalihiyn cha Imam an-
Nawawiy, Hadiyth Namba 150. Jambo
ambalo linaweza kupatikana katika kufuata
Sunnah hii ya funga ambayo ni bora kabisa
ni lazima baada ya kila wiki mbili utakuwa
ni mwenye kufunga siku ya Jumamosi. Na
ikiwa aina hii ya funga imeitwa ndiyo funga
bora na Mtume wa Allah (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) tutaweza
kuitekeleza namna gani?

Juawyriyah bint al-Haarith, Mama wa
Waumini anatuhadithia:
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa
sallam) alinitembelea Ijumaa siku ambayo
ilikuwa nimefunga, akaniuliza: “Je, ulifunga
jana”. Nikasema: “Hapana”. Akauliza tena:
“Je, una nia ya kufunga kesho?” Nikasema:
“Hapana”. Akasema: “Basi fungua” . Katika
riwaya nyingine: “Alimuamuru afungue,
naye akafungua” (Al-Bukhaariy).
Na katika Hadiyth ya Jaabir (Radhiya
Allaahu 'anhu) amesema Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
amesema: “Usifunge siku ya Ijumaa mpaka
uwe umefunga siku kabla yake au siku
inayofuata” (Al-Bukhaariy na Muslim).
Kwa hiyo hapa inaonesha kuwa siku
inayofuata baada ya Ijumaa ni Jumamosi.
Imepokewa kwa Abu Qataadah (Radhiya
Al

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire