Pierre Nkurunzinza janja janja sana huyu
bwana,hata jana nchini mwake hakuondoka
na ndege ya nchi yake...ili kuwapoteza
maboya maadui wake alikodi ndege toka
South Africa ikaja kumchukua Bujumbura -
Dar es Salaam.Hata "Call Sign" yake
haikuwa inaita kama "Burundi 001" ilikuwa
inaita kwa Registration number yake ambayo
ni ya South Africa,maana nasikia alipanda
LearJet45(LJ45) yenye usajili wa ZS-OPR
ambayo ni usajili wa Afrika Kusini
Sasa kama Rais alifikia kukodi ndege toka
Afrika Kusini maanake alianza kunusa harufu
za uasi toka kwa watu wake,ambao pengine
angekuja na ndege ya Serikali kwayo
Marubani wake ni Wanajeshi wangeweza
kumuhujumu kwa namna yoyote ile.Hii
kukodi ndege ya nchi nyingine na
kuendeshwa na marubani ambao ni raia wa
nchi nyingine ya Afrika kusini ndio
imemuokoa jana Rais Pierre Nkurunzinza,laa
sivyo kama angekuwa amekuja na ndege ya
Serikali ya Burundi basi historia ya mwaka
1994 ingejirudia jana ktk uwanja wa ndege
wa Bujumbura kwa Nkurunzinza kuripuliwa
na ndio ingekuwa mwanzo wa machafuko
kati ya wale wanaomuungu Nkurunzinza na
wale wasio watiifu kwake
Kwenye usafiri wa anga kuna kitu wanaita
"Call Sign",huu huwa ni muito wa ndege au
utambulisho wake inapokuwa ktk safari
zake,utambulisho huu unaweza kuwa ni
namba ya usajili ya ndege,au jina la kampuni
ya ndege au jina "mahalia" linaloambatana
na "flight number"...kwa mfano wa jina
"mahalia" kwa ndege za shirika la umma la
Afrika Kusini ni "springbok",huyu ni mnyama
mwenye sifa na heshima kwa S.Africa,British
Airway wao ni "Speedbird",wakati mashirika
kama Fly 540 hujiita kama "swift Tango" n.k
Kwa mfano Tanzania shirika la ndege la fast
jet "call sign" yake hujiita kama "Greybird"
kutokana na picha ya ndege wa kijivu kama
alama ya ndege pale mkiani mwa ndege
zao.Kwa hiyo hata watu mashuhuri duniani
huwa na "call sign" zao wawapo angani au
ardhini iwe tu ni ndani ya ndege,mfano Rais
wa Marekani akiwa ndani ya ndege ya Rais
"call sign" yake huwa ni "Air Force One",
akiwa ndani ya meli ataitwa kama "Marine
One";kwetu hapa Tanzania ndege ikiwa
imebeba rais hujitambulisha kama "Tanzania
One",akiwa makamu wa Rais "Tanzania
Two" na akiwa Waziri mkuu rubani huita
"Tanzania Three".
Tukirudi kwenye mada ya Nkurunzinza
Pierre,jana wakati akiondoka Bujumbura kuja
Tanzania hakujitambulisha kama "Burundi
One" bali marubani wa kukodiwa toka Afrika
Kusini waliita kwa "Call sign" ya "ZS-
OPR",kitu ambacho kilifanywa kuwa siri ya
nani alikuwa ndani ya ndege hiyo,kwa aina
ya usajili wa ndege maadui wa Nkurunzinza
iliwawia vigumu kujua hasa ni nani yupo
ndani ya ndege hiyo na wasingefanya lolote
sababu usajili wa ndege ilikuwa ni Afrika
Kusini.
Mara baada ya mkutano hapa
DSM,Nkurunzinza alitaka kurudi kwa lazima
Bujumbura ili akahutubie Taifa kupitia Radio
na Tv za Serikali,kujiamini kwako kulikuwa na
sababu ya aina ya ndege aliyotumia ili kutua
ktk uwanja wa Bujumbura,kitu ambacho
aliamini maadui zake hawawezi "kuitungua"
kwa sababu zifuatazo:
(1)Ilikuwa ni ndege ya kiraia toka Afrika
Kusini
(2)Ilikuwa ndege inayoongozwa na marubani
raia wa S.Afrika.
Kuitungua ndege hii yenye marubani wa
Afrika Kusini tena "raia" waliombeba "mteja"
aliyeikodi,ingeamsha mgogoro mpya wa
kidiplomasia ambao "maadui" zake
wasingeweza kukubali mtego huo
Nkurunzinza aliondoka Dar es Salaam
milango ya saa 1815hrs,lakini baada ya
kama saa moja na nusu alirudi tena kutua
kwenye uwanja wa ndege wa Dsm,hii ni
baada ya kujaribu kutua mara mbili katika
uwanja wa Bujumbura kwa "Call sign" ya "
ZS-OPR" badala ya "Burundi One".Hata
baada ya rubani kuulizwa mara kadhaa
"status of souls on board" alisisitiza kuwa ni
"customers" waliomkodi toka Bujumbura-
Dsm-Bujumbura.
Baadae Rubani wa ndege akaambiwa "Clear
to land at your own risk"...hii ni baada ya
chumba cha waongoza ndege kuwa tayari
mikononi mwa wanajeshi wasio watiifu kwa
Nkurunzinza,hali hii ilimfanya Rubani
kugeuza na ku-opt Entebbe International
Airport,ambapo Mseven hakuwa tayari,ndipo
Pierre akaamua kurudi kwa "Baba" zake
Tanzania,mpaka sasa hajulikani amefikia
sehemu gani ktk jiji la Dsm,hata Waziri
Membe alipooulizwa leo kuwa Nkurunzinza
yupo Tz sehemu gani,hakutaka kusema
mahali alipo
Hiki ndio kitu pekee kilichomuokoa Brother
Nkurunzinza,vinginevyo maadau zake
waliokuwa wamefunga mipaka na kutawala
viwanja vya ndege wangefanya lolote
endapo tu ndege aliyokuwa anatumia
ingekuwa ni ile ya Rais ambayo huitumia
mara kwa mara,maana kwa maadaui zake
kurudi kwa Nkurunzinza toka Dsm na
kuhutubia Taifa ingekuwa ni pigo kwani
ingezuia vuguvugu na harakati za kumuondoa
madarakani zilizokwisha anza.
Lakini mbadala mwingine kama Nkurunzinza
angekuwa ametumia ndege ya Rais kurudi
Bujumbura kwa kulazimisha ni ima maadui
zake wangeitungua ndege yake au
wangeruhusu itue na kumshikiria Pierre kwa
nguvu,lakini kwa sababu ya "mbeleko" ya
ndege ya "kiraia" yenye marubani " raia"
toka nchi ya Afrika Kusini,Maadui zake
walizingatia diplomasia ya kimataifa na
kumsihi rubani asitue Bujumbura "if and only
among the souls on board,the soul of
Nkurunzinza was boarded"...hii ndio ilikuwa
nafuu ya Bro Nkurunzinza na "ujanja" wa
team yake ya kijasusi,vinginevyo leo
tungekuwa tunaongea mengine na pengine
kama yale ya mwaka 1994 ambapo baada ya
mkutano wa Dsm,watu walipokuwa wanarudi
Makwao wakatunguliwa.
Google tag
samedi 16 mai 2015
Sababu Zilizosaidia Ndege ya Nkurunzinza Isitunguliwe Bujumbura
Inscription à :
Publier les commentaires (Atom)
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire