Google tag

mercredi 14 septembre 2016

Fifa yaitibulia Man Utd kwa Griezmann

                   NADHANI umeshawahi kusikia stori za Gareth Bale na Antoine Griezmann kuhusu kutua Manchester United hapo mwakani,

lakini Fifa imetibua dili mwanangu.
Mabosi wa Manchester United ambao wao kutumia pesa si tatizo, walikuwa na mpango wa kulishika pabaya soka la Hispania kwa kuwanasa mastaa wao muhimu ikiwamo Bale na Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid, Griezmann kutoka Atletico Madrid na Neymar wa Barcelona.

Hata hivyo, sasa Fifa imetibua baada ya kushikilia msimamo wa kuzifungia kusajili Real Madrid na Atletico Madrid kwa madirisha mawili mfululizo ya usajili jambo ambalo litazifanya timu hiyo kusitisha mpango wowote wa kuuza mastaa wao kwa sababu hawataweza kupata wa kuziba mapengo. Atletico Madrid na Real Madrid sasa zitaruhusiwa kusajili kwenye dirisha la Januari 2017.
Kutokana na hilo, staa pekee wa Hispania ambaye Man United wanaweza kulazimisha na kuipata saini yake ni Neymar, ambaye huenda akashawishika kuondoka kwenye timu hiyo kwenda kuanza maisha kwenye timu ambayo atahesabika kama staa mkubwa wa timu tofauti na ilivyo Barcelona ambapo amemezwa na Lionel Messi.
Real Madrid sasa inataka kuwafunga vitanzi mastaa wake kwa kuwapa usajili wa muda mrefu ili kujiondoa kwenye hatari ya kunaswa na timu nyingine wakati ikiwa bado inawahitaji waendelee kubaki Santiago Bernabeu. Kutokana na hilo Man United sasa imeamua kusitisha mpango wa kuwasajili nyota hao pamoja na Neymar wa Barca.
Ripoti kutoka ndani ya klabu ya Man United zimeelezwa kushangazwa pia na taarifa zilizozagaa huko Hispania kwamba, walipanga kumpa Neymar mshahara wa Pauni 650,000 kwa wiki ili aachane na Barcelona.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire