Alibaba

mercredi 14 septembre 2016

INAWEZEKANA: Leicester City walihitaji kusajili mastaa wapya!

NDUGU msomaji, dirisha kubwa la uhamisho lilifungwa wiki iliyopita. Dirisha hilo lilikuwa nafasi kubwa kwa klabu kubwa England kujipanga upya na kuboresha vikosi vyao.
Lakini, wakati klabu kama Manchester City na Manchester United vimekuwa na lengo hilo, la kusajili wachezaji wenye uwezo wa kuboresha vikosi vyao, mabingwa wa England, Liecester wamekuwa na lengo tofauti.
Lengo kuu la timu hiyo katika dirisha kubwa la usajili lilikuwa kuhakikisha kwamba, nyota wa timu hiyo hawauzwi kwenda klabu kubwa zaidi, ambazo zilikuwa zikiwasaka usiku na mchana.
Bila shaka wachezaji kama Riyad Mahrez, N’Golo Kante na Jamie Vardy walikuwa na mchango mkubwa kuhakikisha Leicester wanakuwa mabingwa wa England.
Lakini, bahati nzuri kwa Leicester City ni kwamba kati ya wachezaji hawa watatu, ni Kante tu ambaye alisajiliwa na Chelsea baada ya kupigwa dau la uhakika na kuamua kung’oka klabuni hapo.
Hakika Kante ameacha pengo kubwa katika kikosi cha Leicester kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusoma mchezo na kumudu jukumu lake. Hata hivyo, viongozi wa klabu hiyo wanaamini kwamba, walikuwa na dirisha zuri la usajili kwa kuwa walifanikiwa kumbakisha Vardy na Mahrez.
Wachezaji hawa wawili walisakwa sana na vilabu vingi tofauti katika dirisha kubwa la uhamisho wakiwemo Arsenal. Na bado waliamua kubaki Leicester.
Hivyo, katika karatasi ukimtoa tu Kante, Leicester bado wana kikosi kile kile ambacho kilishinda Ligi Kuu ya England.
Na pia wana kikosi kipana zaidi kutokana na kumsajili Ahmed Mussa kutoka CSKA Moscow.
Lakini, timu hiyo imeanza msimu huu vibaya sana. Wikiendi hii, Leicester walifungwa na Liverpool mabao 4-1.
Na kwa sasa wameshika nafasi ya 15 wakiwa na pointi moja tu baada ya mizunguko mitatu.
Leicester kwa mtazamo wangu hawana kikosi kibaya, lakini tofauti na klabu zingine za England, wameshindwa kuboresha kikosi chao katika dirisha kubwa la usajili. Ndio walifanikiwa kuongeza mkataba wa wachezaji tegemeo kama Vardy na Mahrez.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire