Kocha wa timu ya Taifa ya Togo, Claude LeRoy chupu chupu kuingia jela badala yake amepigwa faini, kwa kuhusika katika uhamisho wa uongo wakati alipokuwa kocha wa Racing Club de Strasbourg, ya Ufaransa.
LeRoy, alikuwa akiifundisha klabu hiyo, kati ya 1998 hadi 2003, aliagizwa na mahakama kuu ya Strasbourg kulipa pauni 12,790 (Takribani shilingi milioni 36.8).
Kocha huyo anadaiwa kujihusisha katika kughushi sahihi na majina ya uwongo katika uhamisho wa wachezaji wanne.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire