Ligi ya Uingereza imetoa orodha
rasmi ya wachezaji 25 watakaochezea kila klabu ya Uingereza katika ligi
kuu msimu wa mwaka 2016-17.
Kuna takriban wachezaji 46 wanaocheza
kulipwa nchini Uingereza msimu huu kutoka Afrika, ikiwa ni ongezeko la
mchezaji mmoja ikilinganishwa na msimu uliopita.Hii ni sawa na asilimia 9 ya jumla ya wachezaji 500.
Kila klabu katika ligi hiyo ina mchezaji wa Kiafrika.
Timu ya Senegal
Timu ya Senegal ndio yenye idadi kubwa ya wachezaji wake katika ligi hiyo,ikiwa na wanane,ikifuatiwa na Ivory Coast yenye wachezaji sita,Nigeria ikiwa na wachezaji watano,Algeria wachezaji wanne huku Ghana ikiwa na watatu.
Taifa hilo lina uwezo wa kutengeza timu yake ya ligi ya Uingereza.
Ina wachezaji kama vile washambulizi,winga,na mabeki.
- Cheikhou Kouyate (West Ham United)
- Diafra Sakho (West Ham United)
- Pape Souare (Crystal Palace)
- Idrissa Gana (Everton)
- Oumar Niasse (Everton)
- Sadio Mane (Liverpool)
- Mame Biram Diouf (Stoke City)
- Papi Djilobodji (Sunderland)
Cha kushangaza ni kwamba hakuna kipa wa Kiafrika miongoni mwa wachezaji hao 45 katika ligi ya Uingereza.
Pengine umtaje kipa wa DRC Steve Mandanda mzaliwa wa Crystal Palace
anayechezea Ufaransa.
Leicester 5 - Sunderland 5
Klabu za Leicester na Sunderland zina idadi kubwa ya wachezaji kutoka Afrika huku kila timu ikiwa na wachezaji 5.
Everton ,Watford na West Ham zinafuatia karibu zikiwa na wachezaji wanne kila upande.
Sunderland ina historia kubwa barani Afrika.
Imezuru mataifa ya waliokuwa wachezaji mashuhuri kama vile Patrick Mboma wa Cameroon,Asamoah Gyan na John Mensah,Benjani Mwaruwari wa Zimbabwe, na Talal El Karkouri wa Morocco.
Mwaka uliopita Crystal Palace ilikuwa na wachezaji wengi kutoka Afrika ,ikiwa na wachezaji watano kwa jumla lakini sasa ina watatu pekee.
Equitorial Guinea na Libya wana wachezaji wao wa kwanza wa ligi ya Uingereza msimu huu kama vile beki Emilio Nsue wa Middlesbrough na Sadik El Fitouri wa Manchester United.
Beki anayelipwa juu zaidi.
Beki wa Ivory Coast Eric Baily ndio baadhi ya mabeki wa kiwango cha juu waliojiunga na ligi ya Uingereza msimu huu.
Uhamisho wake wa kitita cha pauni milioni 30 unamuorodhesha kuwa miongoni mwa mabeki ghali katika ligi hiyo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire