Mwanasheria wa bingwa wa zamani wa mbio za magari, Michael Schumacher, amedai kuwa hatoweza kutembea tena.
Felix Damm alikuwa akiongea kwenye mahakama ya huko Ujerumani kwa niaba ya familia Schumacher, wanaolishtaki jarida moja ambalo liliandika habari kuwa dereva huyo mwenye maika 47 ataweza kutembea tena.
Schumacher, aliyewahi kuwa bingwa wa mashindano ya Formula 1 mara saba, aliumia vibaya wakati akicheza michezo ya kwenye barafu huko Ufaransa mwaka 2013.
Jarida la Bunte la Ujerumani lilidai kuwa Schumacher anaweza kutembea tena, lakini Damm alikanusha vikali kuwa nyota huyo hajapona kiasi hicho. Kwa mujibu wa Mirror, Damm alisema Schumacher hawezi kutembea wala kusimama.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire