Klabu za Borussia Dortmund na Legia Warsaw zilivunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne, kwa kufungana jumla ya mabao 12.
Wajerumani hao chini ya Thomas Tuchel walishinda wapinzani wao kutoka Poland 8-4 mechi ya kusisimua iliyochezewa Ujerumani.
Walivunja rekodi iliyowekwa mabao 11 yalipofungwa mechi ambao Monaco waliwalaza Deportivo La Coruna 8-3 mwaka 2003.
Mabao saba yalifungwa dakika 22 za kipindi cha kwanza.
Legia ndiyo klabu ya kwanza kufunga mabao manne mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na bado kushindwa kwenye mechi.
Rekodi zilizovunjwa
---------------------
* Ni mara ya kwanza historia ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wachezaji wanane kufunga mechi moja
* Dortmund ni klabu ya nne baada ya Liverpool, Monaco na Real Madrid kufunga mabao manane mechi moja Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
* Ilikuwa mechi ya kwanza michuano ya ngazi ya juu Ulaya kufungwa magoli 12 tangu Ajax walipolaza Red Boys Differdange wa Luxemburg 14-0 michuano ya zamani ya Kombe la Uefa 3 Oktoba 1984.
* Ni mechi moja pekee historia ya Kombe la Ulaya na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo mabao zaidi yalifungwa, Feyenoord ya Uholanzi ilipolaza KR ya Iceland 12-2 mnamo Septemba 1969.
* Dortmund sasa wamefunga mabao 14 dhidi ya Legia msimu huu, mabao mengi zaidi kufungwa dhidi ya mpinzani mmoja msimu mmoja wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
* Shinji Kagawa - ambaye wakati mmoja alichezea Manchester United - alifunga mabao mawili katika sekunde 76, mabao mawili ya kasi zaidi historia ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
* Reus arejea kwa kishindo
Marco Reus wa Dortmund alirejea kwa kishindo baada ya kukaa nje kwa miezi sita kutokana na jeraha. Alikuwa na nahodha wa timu na alifunga mabao matatu.
"Nilifurahia kuwa hapo tangu mwanzo," alisema Reus ambaye alikosa Kombe la Dunia 2014 na Euro 2016 kutokana na jeraha.
Mambo yalivyokuwa
------------------
Moja - Legia wajiweka kifua mbele
Mbili - lakini hawaongozi muda mrefu
Tatu - Wajerumani wanaongoza
Nne - nakuongeza jingine
Tano - lakini Legia wanakomboa
Sita - sasa ni 4-2, wataendelea?
Saba - Reus anafanya mambo
Nane - na kisha anafunga jingine
Tisa - watajikwamua?
Kumi - tumefikisha mabao kumi!
11 - umekuwa usiku mrefu?
12- mambo yanamalizika 8-4
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire